Taswira ya daraja la Mtera, ambalo pia hutumika kama milango ya kupitishia maji ya kusukuma mashine za kufua umeme. picha hii imepigwa Desemba 20, 2017.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mtera
UHARIBIFU
wa mazingira unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi na shughuli za
kibinadamu kwenye bwawa la Mtera sio tu unaathiri kiasi cha maji kwa
matumizi ya Kituo cha kufua umeme cha Mtera bali pia unaathiri pakubwa
kituo kingine cha kufua umeme cha Kidatu mkoani Morogoro, Mtaalamu wa
Mazingira wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, Bw. Yusuf Kamote
amewaambia waandishi wa habari waliotembelea Kituo cha Kufua Umeme wa
Maji cha Mtera, kilichoiko mpakani mwa mikoa ya Dodoma na Iringa.
Ukiachilia
mbali mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za kibinadamu kandokando ya
mito, kunachafua mazingira ya mito hiyo na kupunguza kiasi cha maji na
hivyo kuathiri uzalishaji umeme wa maji.
“Tatizo hili ni kubwa
watu wanaingilia mito hii, kuna wakulima na wafugaji wanathiri sana,
shughuli za kilimo na ufugaji zinaleta mchanga mwingi kwenye maji na
hivyo kupunguza kina cha mto na maji yenyewe tunaita siltation, na hiyo
ikitokea ujio wa maji kwenye mitambo unapungua na hivyo uzalishaji
unapungua kama hivi sasa mnavyoona maji yamepungua.” Alisema.
Bw.
Kamote aliwaasa wananchi kuacha kuaharibu mazingira kwani athari zake
ni kubwa katika kuendesha mitambo ya kufua umeme ambao ni muhimu kwa
uchumi wanchi.“Yawezekana wanafanya shughuli hizo kwa kutokujua athari
zake katika uzalishaji umeme, kwa hivyo tunashauri wananchi waelewe
kwamba hilo ni tatizo na waache.” Alisetoa rai Bw. Kamote.
Wahariri wakiangalia jinsi moja kati ya mashine mbili za kufua umeme wa maji inavyofanya kazi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...