Mhasibu Mkuu wa Serikali, Francis Mwakapalila
(kulia), akikabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza wa kipengele cha Wazalishaji
katika tuzo za Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya
Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ya mwaka 2016 kwa Mdhibiti Fedha wa
Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Isaac Lupokela, katika hafla iliyofanyika
jijini Dar es Salaamjuzi. Tanga Cement pia iliibuka na ushindi wa jumla katika
tuzo hizo hii ikiwa ni mwaka wa pili mfukulizo kuibuka na ushindi wa jumla. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA,
Pius Maneno.
Wahasibu wa Tanga Cement, Edgar Mlenge (kushoto), na Isaac Lupokela wakionesha
tuzo ya mshindi wa jumla mara baada ya kampuni yao kutangazwa washindi katika
Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na
Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2016 jijini Dar es Salaam juzi.
Wahasibu wa Tanga Cement, Edgar Mlenge (kulia), na
Isaac Lupokela (katikati), Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa TCPLC,
Mtanga Noor (kushoto), wakionesha tuzo ya mshindi wa jumla na mshindi wa kwanza
kipengele cha Wazalishaji mara baada ya kampuni yao kujizolea tuzo hizo katika
Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na
Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2016 jijini Dar es Salaam juzi.Mdhibiti Fedha wa Tanga Cement, Isaac Lupokela (katikati), akisakata rumba pamoja na baadhi ya waalikwa katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa tuzo za uwasilishaji bora wa mahesabu zilizoandaliwa na NBAA jijini Dar es Salaam juzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...