
Zoezi
hili ambalo linaishia mwezi huu wa Disemba mwishoni.Ili kuwazawadia
wateja wake hususani wale wenye kadi zenye Chip, Umoja switch imeanzisha
droo kubwa inayowezesha wateja kushinda fedha wanazotoa kwenye ATM
maradufu,shilingi milioni moja,simu za mikononi au T-shirts za Umoja.
Droo hii ni kwa wateja wenye kadi mpya ambao wanatumia ATM za Umoja
popote Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja Danfold Mbilinyi alisema “ Lengo kuu la umoja ni kusogeza huduma za kibenki kwa Watanzania wengi zaidi popote Tanzania. Tunafurahi kuwa tumeweza kufika maeneo mengi Nchini na bado tunalenga kuongeza kasi ya ubunifu na usogezaji wa huduma zetu.
Kuboresha
ubora wa kadi zetu ili kuongeza usalama na pia kutoa fursa zaidi ya
ubunifu ni ishara tosha kuwa Umoja Switch inalenga kuwa msharika
madhubuti wa Maendeleo ya Tanzania hususani sekta ya kifedha.
Tunawakaribisha wateja wetu na hata ambao si wateja wetu kubadilish kadi
au kufungua akaunti kwenye benki yeyote mshirika ili nao washinde
kwenye droo hii kubwa“.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...