MWANDISHI wa habari mwandamizi, Mayage Mayage, (56), aliyefariki dunia juzi baada ya kuugua kwa muda anatarajiwa kuzikwa siku ya Alhamis Desemba 28, 2017 katika makaburi ya Mbweni, eneo linaloitwa Maputo', kwa mujibu wa mdogo wa marehemu, Emmanuel Mayage.
Mayage amekutwa na umauti katika Hospitali ya Misheni ya Mbweni, Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa muda wa wiki mbili. Taarifa kutoka kwa mdogo wake Emmanuel Mayage, alisema kuwa madaktari waligundua kaka yake kuugua saratani na kifua kikuu (TB).
Emmanuel amesema kuwa taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwa marehemu Mbweni Kijijini, eneo la Maputo ambako ndugu na jamaa wanakutana.
NAMNA YA KUFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU.
Hapo nyumbani kwake marehemu Mbweni Kijijini eneo la Mbweni Maputo, siyo mbali na hospitali ya Mbweni Misheni.
Ukiwa unatokea Mwenge unapanda daladala ziendazo Mbweni, unashukia kituo cha Mbweni Misheni, kisha hatua chache mbele kuna njia inayokwenda kushoto ituate hiyo kwa kuongozwa vibao vinavyoelekeza kuelekeza msiba ulipo mpaka utakapofika nyumbani kwa marehemu, ambaye ni maarufu kama Mzee wa Magazeti.
Njia nyingine ni kupanda mabasi ya Makumbusho-Bunju/Magamoyo, shukia kituo cha Mianzini Bunju.
Hapo chukua bodaboda kwa gharama ya 3000/= hivi hadi mbele kidogo ya Mbweni Misheni Hospitali. Hapo kata kushoto na muelekeze bodaboda afuate vibao vya kuelekeza msiba hadi nyumbani kwa marehemu.
Kwa wenye usafiri binfsi; unaweza kufika kwa njia mbili:
1.Ukitoka Mwenge nenda mpaka Petrol Station ya Lake Oil eneo la Bunju.Hapo kuna barabara ya lami kuelekea Mbweni.Ifuate hadi Mbweni Misheni Hospitali.Baada ya hapo kata kushoto.Fuata vibao vya msiba.
2.Ukitoka Mwenge nenda hadi njia panda Mbweni,fuata njia ya daladala, pita mageti ya Jeshi hadi Mbweni Kijijini.Endelea mbele hadi Mbweni Misheni Hospitali.Sogea mbele kidogo, halafu kata kushoto na anza kufuata maelekezo ya vibao vya msiba.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMIN
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMIN
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...