Ntegenjwa Hosseah, Mpwapwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amesema vituo vyote 211
vinavyoongezewa miundombinu ya Afya vinahitaji wataalam wa kutoa Dawa za Usingizi ili
kukidhi mahitaji ya wagonjwa watakaofikishwa katika chumba cha Upasuaji pamoja na Wodi
ya Kinamama.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya Kikazi Wilayani Mpwapwa na
kukagua miradi ya maendeleo iliyompelekea kufika katika ujenzi wa miundombinu ya Afya
inayojengwa katika Kituo cha Afya Mima.
Akiwa kituoni hapo alisema ameridhishwa na ujenzi wa miundombinu hiyo ambapo hii ya
awamu ya kwanza itakamilika mapema Mwezi Januari 2018 lakini anaona uhitaji wa
wataalam wa kutoa Dawa za Usingizi ambao watatoa huduma hizo wakati wa upasuaji na
huduma nyingine muhimu.
“Nataka vituo hivi vinapokamilika vianze kufanya kazi mara moja na sio zianze sababu mara
wataalamu Fulani hakuna hiki bado sitapenda kusikia hayo ni vyema kwa sasa kila
Mkurugenzi wa halmashauri ahakikishe anabainisha wataalam angalau wawili ambao
watakwenda kupata mafunzo mafupi ya utoaji wa Dawa hiyo ya Usingizi wakati wa Upasuji”.
Mpaka sasa nimeridhishwa kabisa na kasi ya Ujenzi wa vituo hivi vya Afya na kwa sababu
vifaa Tiba pia tunapata kutoka Bohari Kuu ya Dawa sasa kwa pamoja tuangalie maeneo
mengine ambayo yataenda sambamba na utoaji wa huduma katika vituo hivi kama
wataalamu hawa ambao kwa Takwimu zilizopo kwa sasa bado ni wachache na baada ya
ukamilishwaji wa vituo hivi Uhitaji Utakua Mkubwa zaidi alisema Waziri Jafo.
Awali akitoa Taarifa ya Ujenzi Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Space East Africa iliyopewa
Kazi ya Kujenga Kituo cha Afya Mima Gaston Francis amesema kampuni hiyo hujenga kwa
kutumia Teknolojia ya Kisasa iitwayo “Pre-Fabricated Material” ambayo ni nafuu zaidi na ina
ubora wa hali ya juu hivyo kwa gharama hiyo ya Mil 500 watajengwa majengo saba huku
yakiwa na thamani zote zinazohitajika “Full furnished”.
Aina hii ya Teknolojia hutumika sana maeneo yenye vimbunga, upepo Mkali na Dhoruba
mbalimbali na kwa sababu eneo hili la Mima linaathiriwa sana na wadudu Material hii
tunayotumia itaenda kuwa suluhisho la kudumu la wadudu hao kwa sababu hawataweza
kuathiri hata eneo moja na majengo tutakayojenga na ubora wa material hizi tunazotumia
zinadumu kwa Zaidi ya miaka sabini alisema Francis.
Awali katika ziara yake Waziri Jafo alianza kwa kutembelea ujenzi wa barabara ya Lami ( Km
1 ) iliyojengwa kuanza NMB Mpwapwa mpaka Stendi ya Mpwapwa, kukagua Mradi wa Maji
Mima pamoja na kuzungumza na wananchi wa Mima kwenye Mkutano wa hadhara.
Mbunge wa Mpwapwa Mhe. George Malima Lubeleje(kushoto) akielezea Umuhimu
wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa hivi katika sasa kwa Waziri wa
Nchi, OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani
Jafo (kushoto) akimskiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Space East Africa
Gaston Francis(Kulia) namna wanavyojengwa kwa kutumia Teknolojia ya “Pre
Fabricated Material’.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani
Jafo(kushoto) akikabidhiwa kitendea kazi ili aweze kushiriki kwenye Ujenzi wa Kituo
cha Afya kwa kutumia Teknolojia ya “Pre Fabricated Material”.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani
Jafo(aliyeinama) akishiriki kukata chuma kitakachotumika katika ujenzi wa jengo la
Maabara kwa kutumia Teknolojia ya “Pre Fabricated Material”.
Hili ni moja ya Jengo lililojengwa katika Kituo cha Afya Mima kwa Kutumia Teknolojia
ya “Pre Fabricated Material” linalojengwa na Kampuni ya Global Space East Africa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...