Wananchi
wa Wilaya ya Gairo wameombwa kuendelea kujitoa kwa hali na mali katika
maendeleo ya sekta ya elimu ili kupata matokeo bora.
Kauli
hiyo imetolea Disemba 21, 2017 wakati wa kuwasomea mapato na matumizi
ya michango ya elimu kwa wananchi wa Kata ya Chakwale na Mkuu wa Wilaya
ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe wakati akabidhi tani mbili na nusu
ya mifuko ya saruji kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno.
Mhe. Mchembe
alisema kuwa saruji hiyo itasaidia kuendeleza zoezi la kufyatua matofali
ambapo mpaka sasa wameshafyatua matofali 5,600. Aidha amekaribisha
wadau mbalimbali kuendelea kuchangia baada ya wananchi kuchangia
shilingi milioni 33 ndani ya miezi mitatu.
"Hamasa
ni kubwa kwani watoto wanatembea kilometa zaidi ya Sita kwenda shule.
Hili limekuwa ni jaribu kwa watoto wa kike. Vijana wa bodaboda
wanatuharibia watoto wa kike. Shule ikiwa karibu itapunguza changamoto
hii.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akimkabidhi mifuko ya saruji kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno ili iweze kusaidia katika ujenzi wa madarasa, ofisi za walimu na nyumba za walimu. Mkutano huo ulifanyika Disemba 21, 2017 katika Kata ya Chakwale, Gairo.

Wananchi wa Kata ya Chakwale wakisomewa taarifa ya michango yao shilingi milioni 33. Aidha Wenyeviti wa vijiji vitatu walirudishiwa shilingi milioni 10 ikiwa ni kwa ajili ya shughuli za Maendeleo ya vijijini.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akikabidhi hundi ya milioni kumi kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno ili awagawie Wenyeviti wa kata yake. Mkutano huo ulifanyika Disemba 21, 2017 katika Kata ya Chakwale, Gairo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...