Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa 16 ya Tanzania ambayo zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa linaendelea huku mamia ya wananchi wakionekana kuhamasika na zoezi hilo kwa kujitokeza kwa wingi kwenye vituo ambavyo usajili umekuwa ukiendelea.

Akizungumzia zoezi hilo Afisa Usajili wa Wilaya ya Kahama bwana Ibrahim amesema mwitikio mkubwa wa watu katika vituo vya usajili ni kiashiria kwamba uelewa wa wananchi ni mkubwa na kwamba wanatambua vitakavyowasaidia katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Akizungumzia gharama za zoezi afisa huyo ameeleza zoezi ni BURE na kwamba mwananchi hapaswi kutozwa kiasi chochote cha fedha zaidi ya kufika na nakala (photocopy) za nyaraka/viambatanisho muhimu vya kuweza kumtambulisha uraia wake, umri na makazi. Mfano wa nyaraka hizo ni; Kadi ya mpiga kura, cheti cha kuzaliwa, leseni ya udereva, ID ya Mzanzibar mkazi, TIN, Pasi ya kusafiria, vyeti vya elimu nk.

Mbali na Shinyanya mikoa mingine ambayo NIDA inaendesha zoezi ni Iringa, Mara, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Songwe, Njombe, Singida, Manyara, Mwanza, Simiyu, Mara, Geita, Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akimsajili mmoja wa Wananchi wa Kata ya Kahama Mjini aliyejitokeza kusajiliwa wakati zoezi la usajili likiendelea kwenye Kata hiyo.
Mkusanyiko wa wananchi wa Kata ya mjini Wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakisubiri huduma ya usajili Vitambulisho vya Taifa, zoezi linaloendelea katika Wilaya hiyo na kuhusisha Kata ya Mjini na mitaa yake.

Mkusanyiko wa wananchi wa Kata ya mjini Wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakisubiri huduma ya usajili Vitambulisho vya Taifa, zoezi linaloendelea katika Wilaya hiyo na kuhusisha Kata ya Mjini na mitaa yake.

Mmoja wa wananchi wa Kahama akisajiliwa na kujaziwa fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa na Mtendaji wa Mtaa wa Kahama kabla ya kusajiliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...