Na; Shamimu Nyaki-WHUSM.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka Wasanii wote hapa Nchini kuwa wabunifu na kutumia weledi katika kutengeneza kazi zenye ubora wa hali ya juu kwakua ndio utakaowasaidia kupata soko la uhakika.

Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizindua Kanzi Data ya wasanii iliyoandaliwa na Taasisi ya Muziki hapa nchini (TAMUF) iliyodhaminiwa na Kampuni ya CogsNet Technologies lengo ikiwa ni kusajili wasanii pamoja na kazi zao ili watambulike na wafaidike kupitia kazi hizo, lakini pia kuendelea na harakati za kupambana na wizi wa kazi za wasanii.

“Nawashukuru sana CogsNet pamoja na TAMUF kwa kuja na wazo hili lenye lengo la kulinda kazi za wasanii,naamini Kanzi Data hii italeta mafanikio kwa wasanii endapo watajisajili na kutengeneza kanzi bora zitakazowapatia soko la uhakika ndani na nje ya nchi”Alisema Dkt.Mwakyembe.

Aidha ameipongeza Taasisi hiyo kwa kuwatafutia wasanii Huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo Bima ya Afya inayotolea na mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF lengo ikiwa ni kuwasaidia wasanii kupata huduma ya afya kwa bei nafuu pamoja na mafao mengine yanayotolewa na Mfuko huo lakini pia akiwataka wasanii kuacha tabia ya kuuza Haki Miliki zao.
Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kutunza taarifa za wasanii wa muziki (Kanzi Data) leo Jijini Dar es Salaam. Mfumo huo unatengenezwa kwa ubia baina ya Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) na Kampuni ya CogsNet Technologies ya hapa nchini.
Rais wa Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) Dkt. Donald Kisanga akielezea jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kutunza taarifa za wasanii wa muziki (Kanzi Data) leo Jijini Dar es Salaam. Mfumo huo unatengenezwa kwa ubia baina ya Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) na Kampuni ya CogsNet Technologies ya hapa nchini.Kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa COSOTA Bi. Doreen Sinare, Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mungereza, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea risala ya Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) kutoka kwa Rais wa mfuko huu Dkt. Donald Kisanga wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kutunza taarifa za wasanii wa muziki (Kanzi Data) leo Jijini Dar es Salaam. Mfumo huo unatengenezwa kwa ubia baina ya Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) na Kampuni ya CogsNet Technologies ya hapa nchini. Kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa COSOTA Bi. Doreen Sinare na Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mungereza.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...