Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Klabu ya Yanga imeuanza rasmi mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji kwa kumteua Wakili Alex Mgongolwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo..

Mgongolwa atasaidiwa na wajumbe watano ambao ni Mheshimiwa Said Mecky Sadick, Profesa Mgongo Fimbo, Felix Mrema, George Fumbuka na Mohammed Nyengi.

Kamati hiyo imetangazwa leo Ijumaa na Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Boniface Mkwasa ikiwa ni siku chache tu tangu watani wao Simba kupitisha mchakato huo na kumpata mwekezaji ambaye alishinda zabuni hiyo.

Yanga wao wamefuata Katiba yao ya mwaka 2010 inayoelekeza kuwa mwekezaji ni lazima awe na asilimia 49 na 51 ziwe za wanachama kwa maana ya klabu kama serikali ilivyofanya mabadiliko ya Katiba katika kipengele cha mfumo wa uendeshaji wa Hisa.

Mbali na hilo Kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga iliyokukutana jana hii tarehe 21/12/2017 makao makuu ya klabu hiyo katika kikao maalumu,imeteua majina 28 ya wanachama kuunda kamati mpya ya mashindano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...