Na Bashir Nkoromo.
Mwenyekiti
mpya wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa ameahidi kuunda
Kamati ya kutathmini namna Jumuiya hiyo inakavyolishughulia kwa ufanisi
tatizo la kuporomoka kwa maadili katika jamii hapa nchini.
Dk. Mndolwa ametoa ahadi hiyo leo, hayo wakati akikabidhiwa rasmi Ofisi na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mstaafu Abdallah Bulembo, hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Jumuiya ya Wazazi Tanzania jijini Dar es Salaam.
"Katika hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli alitutaka sisi viongozi wa Jumuiya hii tusikae kimya wakati vitendo vya kuporomoka kwa maadili katika jamii ikiwemo wasanii wa kike kuonyesha sehemu za miili yao zinazotakiwa kusitiriwa. Sasa hili ni agizo lazima mimi na viongozi wenzangu tulipe kipaumbele katika kulifanyika kazi.
Kwa hiyo baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi leo hii, miongoni mwa mipango yangu Kama Mwenyekiti ni Kuunda Kamati itakayojikita kwa undani kuhakikisha tunapata njia bora za kudhibiti kuporomoka kwa maadili katika jamii ya Watanzania", alisema Dk Mndoldwa. Alisema, pia atahakikisha katika zama za uongozi wake, Jumuiya ya Wazazi inainuka na kujitegemea vya kutosha kiuchumi ili iondokane na adha ya kuwa ombaomba.
"Jumuiya hii ianazo mali nyingi, kinachotakiwa hapa ni kuhakikisha fedha zinazotokana na mali au miradi hii zinaingia kwenye hazina ya Jumuia badala ya kupotelea mifukoni mwa wajanja wachache, tukifanikiwa kuthibiti bila shaka tutakuwa na fedha za kutosha", alisema Dk. Mndolwa.
Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Abdallah Bulembo (kushoto) akikabidhi nyaraka zenye orodha ya mali za Jumuiya hiyo kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo, Dk. Edmund Mndolwa, leo Januari 2, 2018, Makao Makuu ya Jumuiya jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Zanzibar Abdallah Haj Haidar.
Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Wqzazi Tanzania Abdallah Bulembo akionyesha Katiba ya Jumuiya hiyo kabla ya Kumkabidhi Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hizo Zanzibar Abdallah Haj Haidar
Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Abdallah Bulembo (kushoto) akikabidhi nyaraka zenye orodha ya mali za Jumuiya hiyo, kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo, Dk. Edmund Mndolwa, leo Januari 2, 2018, Makao Makuu ya Jumuiya jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Seif Shabani Mohammed na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Zanzibar Abdallah Haj Haidar.
Dk. Mndolwa na Bulembo wakisaini nyaraka za makabidhiano
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...