Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 

SERIKALI ya Tanzania na Global Fund wamewekeana saini mkataba wa Dola za Marekani milioni 525 sawa na Sh.Trilioni 1.155 kwa lengo la kufadhili shughuli za kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu,Maralia na uimarishaji wa mifumo ya afya nchini. 

Imeelezwa ushirikiano huo wa Global Fund ambao ndio waliotoa fedha hizo kwa Serikali ya Tanzania unategemewa kuongeza kuongeza idadi ya Watanzania wanaonufaika na huduma za afya Katina magonjwa hayo. 

Wakati wa utiwaji saini wa mikataba ya fedha hizo, wadau mbalimbali walihudhuria ambao ni viongozi wa Serikali, mabalozi, asasi za kiraia za ndani na za kimataifa.Pia wajumbe wa bodi ya uratibu ya Global Fund nchini pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo ndiyo iliyoandaa shughuli hiyo. 

Akizungumza mapema jana jijini Dar es Salaam baada ya utiwaji saini wa mikataba ya fedha hizo, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Global Fund wamekuwa wachingiaji muhimu katika sekta ya afya.

Amefafanua wamekuwa wachangiaji wakubwa katika kuzuia na kupambana na magonjwa hayo matatu tangu kuanzishwa kwa mfuko huo mwaka 2001."Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania napenda kutoa shukrani za dhati kwa Global Fund kwa ushirikiano wao ambao umewezesha nchi kuboresha afya za wananchi wetu pamoja na kuboresha mifumo ya afya, "amesema Mwalim. 

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora (kulia), na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban, wakisaini hati za makabidhiano ya sh.  trioni moja zilizotolewa na Shirika la Global Fund kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia mapambano ya Ukimwi, TB na Malaria katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo. Wengine waliosimama katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na viongozi wengine kutoka Global Fund.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Mpoki Ulisubisya, akizungumza katika hafla hiyo.
Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania, Frederic Clavier, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban (kulia), akimkabidhi hati ya makabidhiano Mwakilishi wa Global Fund Tanzania, Linden Morrison.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora, akizungumza.
Taswira ya ukumbi wa mkutano katika uzinduzi huo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...