Said Mwishehe,Globu ya jamii
MAWAZIRI wa wizara nne tofauti wameamua kufanya jitihada za kuondoa changamoto ya utoaji huduma kwa muda mrefu na kusababisha msongamano wa wageni wanaiongia na kutoka nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijijini Dar es Salaam.
Pia kuondoa changamoto ya joto katika eneo la kuchukulia mizigo pamoja na kushughukikia hati za kusafiria kwa wageni wanaoingia nchini pamoja na changamoto ya ufinyu wa eneo la kusubiri huduma uwanjani hapo.
Mawaziri hao ambao wamekutana leo katika uwanja huo na kukagua shughuli za utoaji huduma ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala,
Wengine ni Waziri wa Mambo ya Ndani Dk.Mwigulu Nchemba na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dk.Susan Kolimba na Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye. Akizungumza baada ya kufanya ziara hiyo,Waziri wa Mambo ya ndani Ndani Dk.Nchemba amesema kuwa jitihada mbalimbali zinafanywa kutatua changamoto hizo.
Ametaja hatua ambazo wizara yake inachukua ni kuharakisha utoaji huduma wa hati za kusafiria kwa njia ya kieletroniki. Pia wameamua kuongeza idadi ya madawati ya kutolea huduma kwa wageni ikiwa sambamba na kuongeza watoaji huduma ili kurahisisha utoaji huduma wa muda mfupi.
“Taarifa zinaonesha kuwa kwa sasa kuna unafuu mkubwa wa kutoa huduma kwani badala ya saa tatu ambazo zilikuwa zinatumia awali hivi sasa muda wa utoaji huduma umeshuka hadi saa moja.Lengo letu ni kushuka zaidi

Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza na Naibu
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye
(kushoto) wakati walipofanya ziara ya kukagua Changamoto mbalimbali
zilizopo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
jijini Dar es salaam leo. Wengine ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.
Hamis Kigwangala (katika) na kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba
wakisikiliza.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa Dkt. Susan Kolimba akizunumza na waandishi wa habari baada ya
kukamilika kwa ziara ya kukagua changamoto mbalimbali katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es salaam leo
kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt.Anna Peter
Makakala
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala (katikati) akiongozana na
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda
na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba (kushoto) na, Naibu Waziri wa Ujenzi,
Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia)
Kutoka
kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba, Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa Dkt. Susan Kolimba, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis
Kigwangala, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi
Atashasta Nditiye na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Richard Mayongela wakitafakari jambo wakati wa ziara ya kukagua
changamoto mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam leo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala akizungumza na waandishi
wa habari leo mara baada ya kukagua changamoto mbalimbali katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam leo
wengine ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba, Naibu
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye na
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda
na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...