Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imeahidi kuwasaidia wanafunzi wanasoma kozi ya Multi Media kupata nafasi za mafunzo kwa vitendo katika sehemu mbalimbali pale inapowawia vigumu kupata nafasi hizo.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipotembelea Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa lengo la kufahamu kozi ya Multi Media inayotolewa na chuo hicho namna gani inaweza kusaidia uandaaji wa filamu nchini.
‘’Kozi hii ya Multi Media ni moja ya masomo yanaweza kuisaidia sekta ya filamu kupata taswira mpya tofauti na ilivyosasa kwani wataalamu hawa wakitumiwa vizuri katika kuandaa filamu za hapa nchini wanaweza kuleta mabadiliko kwani kwa sasa sekta hiyo ina changamoto kubwa ya kukosa waandaji wenye weledi’’Dkt.Mwakyembe.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) akipongeza uongozi wa chuo cha Teknolojia Dar es Salaam kwa kuaandaa vijana wenye weledi katika uandaaji wa filamu alipotembelea chuo hicho jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kukutana na wanafunzi wanaosoma kozi ya Multi Media,kutoka kulia ni Mkuu wa Chuo cha DIT Prof.Preksedis Ndomba na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bibi. Joyce Fissoo (kushoto).
Mkuu wa Chuo cha DIT, Prof.Preksedis Ndomba (kulia) akitoa taarifa ya maendeleo ya kozi ya Multi Media inayotolewa na chuo hicho inavyoweza kusaidia sekta ya filamu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) alipotembelea chuo hicho jana jinini Dar es Salaam kujionea namna kozi ya Multi Media inaweza kusaidia sekta ya filamu katika uandaaji.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Bibi Joyce Fissoo akiuliza swali kwa baadhi ya wanafunzi wanasoma kozi ya Multi Media katika Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (hawapo pichani) namna gani wanaweza kuboresha uandaaji wa filamu, katika ziara ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) chuoni hapo jana jijini Dar es Salaam (watatu kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha DIT Prof.Preksedis Ndomba.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea chuo hicho kwa ajili ya kufahamu kozi ya Multi Media inavyoweza kusaidia sekta ya Filamu nchini, na wapili kulia ni Mkuu wa Chuo cha DIT Prof.Preksedis Ndomba pamoja na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini Bibi Joyce Fissoo (wapili kushoto). Na Anitha Jonas –WHUSM
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...