Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde leo amezindua
kampeni ya upandaji miti milioni moja katika kijiji cha
Ibwagwa,Wilayani Kongwa Dodoma ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya
KIJANISHA DODOMA iliyozinduliwa na Mhe. Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu
Hassan.
Waziri Mavunde amewataka wananchi wa Kongwa kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kupanda miti mingi zaidi na kuwataka kuacha tabia ya kukata miti ambayo hali inayosababisha uharibifu wa mazingira mkubwa.
Aidha Mavunde ametumia nafasi hiyo kuutaka uongozi wa Wilaya ya Kongwa kuhakikisha kwamba unasimamia utekelezaji wa sheria na kanuni mbalimbali za Mazingira ili kuinusuru wilaya hiyo na uharibifu wa Mazingira.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mkuu wa Wilaya wa Kongwa Mhe. Deogratious Ndejembi amemuhakikishia Naibu Waziri Mavunde kwamba kama watahakikisha miti yote iliyopandwa inastawi ili kufikia lengo la kui-KIJANISHA DODOMA na pia ameahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika kuharibu mazingira hasa kwa ukataji miti na uchomaji wa misitu.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti milioni moja katika kijiji cha Ibwagwa,Wilayani Kongwa Dodoma

Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratious Ndejembi akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti.

Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratious Ndejembi akipanda mti katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akiwa ameshika miche kwa ajili ya kupanda.

Miti inayopandwa katika wilaya ya Kongwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...