Na Agnes Francis, Globu ya Jamii
KOCHA Mkuu wa kikosi cha Real Madrid, Zinedine Zidane ameendelea kusakamwa na matokeo mabaya anayoyapata baada ya jana kuondolewa kwa jumla ya mabao 2-2 dhidi ya Leganes.
Matokeo hayo yameifanya Madrid kuondolewa katika michuano ya Kombe la Mfalme(Copa del Rey).Mtanange huo uliopigwa Uwanja wa Santiago Bernabeu, Madrid imeondolewa kwenye michuano hiyo licha ya ushindi walioupata wakiwa ugenini wa bao 1 - 0 wakati jana Madrid walipokea kichapo cha bao 2 - 1 bila ya nyota wake Christian Ronaldo na Gareth Bale.
Mabao ya Leganes yalipachikwa nyavuni na Javier Eraso na la pili lilifungwa na Gabriel Appelt Pires dakika ya 55,wakati mshambuliaji wa Real Madrid Karin Benzema alipatia timu yake bao dakika ya 47.
Hivi karibuni kabla ya mechi hiyo Kocha Zidane amekuwa akisakamwa na baadhi ya viongozi wake kutokana na mwenendo mbovu wa klabu hiyo siku za usoni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...