Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
MGOMBEA ubunge Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam kupitia Tanzania Labour Party(TLP), Dk. Godfrey Malisa ameomba wananchi wa jimbo hilo kuendelea kuamini kuwa upinzani bado uko imara na kuwataka kujitokeza kwa  wingi na kumpigia kura  ili kuhakikisha jimbo hilo linabaki katika mikono ya upinzani kama walivyokuwa wameaminiwa hapo awali.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Dk.Malisa amesema TLP iko imara na kitahakikisha kinatatua kero zote za jimbo la Kinondoni na kuwaomba wananchi kurudisha imani yao kwao licha ya kuonesha kukerwa kwao na kitendo cha Mbunge wa CUF Maulid Mtulia ambaye wapinzani walimchagua kwa nguvu zote katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 kuhamia Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Amesema, katika kipindi cha siku saba ambacho wanaendelea na kampeni zao, wananchi wamekuwa wakimlalamikia  na kumueleza kuwa wamekerwa na kitendo cha Mbunge wa CUF kuhamia CCM na hata kufukia kumuuliza  iwapo watamchagua nae si anaweza kwenda huko huko kama hao wanaosikia wanahama kila siku.

Aidha amesema, Chadema siku za nyuma walishasema hawatasimamisha mgombea kwenye chaguzi ndogo kutokana na kutokuwa na imani na Serikali lakini cha kushangaza safari hii wameamua kusimamia mgombea kwenye jimbo hilo.

Ameeleza kitendo cha Chadema kumsimamisha mgombea Salum Mwalimu kimewaathiri na zaidi kimeonesha kutokuwa na misimamo kwenye mambo wanayowaambia wananchi.

“Kurudi kwao kunatuathiri sana kwani watanzania watakuwa hawatuamini, yaani wapiga kura wataona sisi wapinzani hatuaminiki, hatueleweki kwani tunapoongea inaonekana tunaongea uongo,"amesema Dk.Malisa.

Ameongeza akichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Kinondoni kipaumbele chake cha kwanza ni  la vijana na ujasiriamali kwani ni eneo lenye changamoto nyingi na kusisitiza atatumia nafasi yake kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kupitia chama cha TLP, Dk. Godfrey Malisa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...