Meneja wa Dula la Phone One, Saiyed Shabi lililoko Mlimani City
akichagua kuponi ya mshindi wa kwanza wa droo ya tatu ya
promosheni ya fanya manunuzi MLIMANI city na ushinde katika msimu
wa sikukuu ijulikanayo kama “Mlimani City Grand Fest” iliyofanyika
mwishoni mwa wiki Mlimani City.Wengine waliomzunguka ni mabalozi
wa promosheni hiyo.
Moja ya watejawa Mlimani City, Swaibu Swalehe akichagua kuponi ya
mshindi wa kwanza wa droo ya tatu ya promosheni ya fanya manunuzi
MLIMANI city na ushinde katika msimu wa sikukuu ijulikanayo kama
“Mlimani City Grand Fest” iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mlimani
City.Wengine waliomzunguka ni mabalozi wa promosheni hiyo.
MWAKA 2017,jumla ya Shilingi milioni 6 zimegawiwa kama
zawadi kwa wateja waliofanya manunuzi Mlimani City tangu
promosheni ya fanya manunuzi mlimani City na ushinde
ijulikanayo kama “Mlimani City Shopping Fest” inayoendelea
katika kipindi hiki cha msimu wa siku kuu ya Krismas na Mwaka
mpya.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Mlimani City,
Pastory Mroso alisema jumla ya wateja 60 mpaka sasa
wameshajishindia kila mmoja vocha yenye thamani ya Shilingi
100,000.Tumeshafanya droo tatu mpaka sasa na kila droo
tulikuwa tunatoa washindi 20, ambapo kila mmoja alijishindia
vocha yenye thamani ya shilingi 100,000 ambapo jumla ya
zawadi mpaka sasa ni shilingi milioni 6 tangu kampeni hii ianze.
Alisema Mroso, ni rahisi sana kushinda, ni wewe kuja mlimani
City na kufanya manunuzi kwenye duka lolote na kwa bidhaa
yoyote ukitumia kiasi cha shilingi 100,000 au zaidi utapewa
kuponi ambayo itakuwezesha moja kwa moja kuingia kwenye
droo ya kushindania zawadi ya vocha yenye thamani ya shilingi
laki moja ambayo itakuwezesha kwenda kufanya manunuzi tena
duka lolote la ndani ya Mlimani City.
Wewe ambaye hujashiriki nafasi unayo bado kuna droo mbili
mbele njoo ufanye manununuzi Mlimani City katika katika kipindi
hiki cha sikuu ya Krismas na mwaka mpya na ushinde.Tunayo
droo ya kubwa ya mwisho ambayo mshindi mmoja atajishindia
vocha yenye thamani ya milioni 10 na washindi wengine watano
watajishindia vocha yenye thamani ya milioni moja kila mmoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...