Na Ripota wa Globu ya Jamii Kagera.

WATU 11 wamefariki Dunia na wengine sita kujeruhiwa kutokana na ajali ya gari aina ya hiace kugongana na malori matatu iliyotokea mnamo majira ya saa tano usiku wa kuamkia leo,katika kijiji cha Mubigera kata ya Nyantakara wilaya ya biharamulo mkoani kagera ,wakati wakisafiri kutoka wilaya ya kibondo kuelekea kahama mkoani Shinyanga.

Mganga mkuu wa hospitali teule ya Biharamulo Dr Grasmus Sebuyoya amethibitisha kupokea miili ya watu hao wakiwa maiti na majeruhi sita na kwamba kati ya majeruhi hao wawili hali zao ni mbaya na waliofariki wa jinsia ya kiume ni saba na jinsia ya kike ni watatu

Dr Sebuyoya amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Juma Samo (25) Joseph Otieno (30), Oscar Leonard Sebastian (27), Baseke Mashinga Nyabashiki (31), Mahalulo Charles (25) na majeruhi wa sita hajafahamika kwa kuwa hajajitambua na kwamba maiti waliofia eneo la tukio ni Tisa na wawili wamefariki baada ya kufikishwa hospitalini hapo.

Awali Mwenyekiti wa kijiji cha Mubigera Bw Mapunda Kayuki amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya Saa 11 jioni ambapo hiece ilitaka kukwepana na roli kwenye barabara ya biharamulo kwenda kahama kwenye kijiji hicho na kugongana ambapo dereva wa hiece na tingo wake ni miongoni mwa waliofariki

Bw Kayuki amesema hiece hiyo yenye  namba za usajili T.542 DKE ilikuwa ikitokea kibondo kwenda kahama ambapo maroli yaliyohusika kwenye ajali hiyo ni T.860CGS, T.103 DUJ na T.147 DUJ magari  yako chini ya usalama wa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amesema hajakamilisha taarifa kamili ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kutambua majina ya waliopoteza maisha mpaka ajiridhishe na taarifa,  zitatolewa kwa umma bila kutia mashaka ili ndugu wa marehemu waweze kujua na kufuatilia kwa uhakika

Ajali ya gari dogo(hiyace)aina ya Nissan caravan yenye usajili wa no.T 542 DKE limegonga na magari makubwa mawili ya mizigo yenye namba za usajili T 694 COX na T 103 DKJ Mali ya kampuni ya Mruruma Enterprinces wa Dar es salaam katika eneo la Ngangozi kata ya Nyantara Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera na kusababisha vifo vya abiria 11 na majeruhi watano

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...