Na Mathias Canal, Dodoma
Sekta ya Madini inachangia kati ya asilimia 3.5 mpaka 4 katika Pato la Taifa ukilinganisha na sekta zingine ambazo zimejitutumua kwa kiasi kikubwa katika mchango mahususi wa pato la Taifa nchini Tanzania.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko amebainisha kuwa kiasi cha kati ya asilimia 3.5 mpaka 4 ni kidogo sana ukilinganisha na umuhimu wa sekta hiyo nchini hivyo Wizara ya Madini imekusudia kuongeza tija katika mchango wa pato la Taifa kupitia sekta hiyo muhimu ya Madini.
Mhe Biteko amebainisha hayo Leo Januari 15, 2018 wakati akizungumza na wakuu wa idara na vitengo pamoja na watumishi wa Wizara ya Madini ofisi Kuu Mjini Dodoma huku akiwataka watumishi wote kufanya kazi kwa bidii, nidhamu na uzalendo mkubwa kwa manufaa ya Taifa.
Alisema kuwa sekta ya Madini ni muhimu nchini kutokana na rasilimali Madini ilizonazo hivyo watumishi wote wanapaswa kufikiria namna ya kufanya kazi kwa tija ili kuwa na ongezeko la mchango mkubwa katika pato la Taifa.
"Natamani nione kwenye taarifa ya robo mwaka ya BOT ikisoma kwamba sekta ya madini inachangia angalau asilimia 10 ya Pato la Taifa kuliko ilivyo hivi sasa na hilo naamini linawezekana kwa ushirikiano wa pamoja" Alisisitiza Mhe Biteko
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akizungumza na wakuu wa idara na vitengo pamoja na wafanyakazi wote wa wizara ya madini mara baada ya kuwasili ofisini Mjini Dodoma, Leo Januari 15, 2018. Picha Zote Na Mathias Canal.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakuu wa idara na vitengo pamoja na wafanyakazi wote wa wizara ya madini mara baada ya kuwasili ofisini Mjini Dodoma, Leo Januari 15, 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Stanislaus Nyongo akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri mwenzake katika Wizara hiyo Mhe Dotto Mashaka Biteko kuzungumza na wakuu wa idara na vitengo pamoja na wafanyakazi wote wa wizara ya madini mara baada ya kuwasili ofisini Mjini Dodoma, Leo Januari 15, 2018.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...