Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Januari, 2018 ametia saini kitabu cha maombolezo na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga (pichani) nyumbani kwa marehemu Oysterbay Jijini Dar es Salaam. 
Mhe. Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pia wametoa mkono wa pole kwa mke wa Marehemu Mama Maria Kisanga na kufanya maombi ya pamoja na familia ya marehemu. 
Jaji Mstaafu Robert Kisanga alifariki dunia tarehe 23 Januari, 2018 katika hospitali ya Regency Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa  Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 208.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimfariji mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakifanya maombi pamoja na mjane wa marehemu Mama Maria Kisangana mtoto wa marehemu Amani Kisanga na waombolezaji wengine baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...