Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Wallace Karia ameteuliwa kwa mara nyingine na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF kuwa kamishna wa mechi ya Morocco na Namibia kwenye fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN itakayochezwa kesho Jumamosi Januari 27, 2018.
Mbali na Rais Karia, Waamuzi watakaochezesha mchezo huo namba 22 utakaochezwa kwenye Uwanja wa Mohamed V Casablanca ni Mahamadou Keita kutoka Mali atakuwa mwamuzi wa katikati akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja kutoka Msumbiji Arsenio Chadreque Maringula na mwamuzi msaidizi namba mbili akitokea Burkina Faso Seydou Tiama wakati mwamuzi wa akiba ni Ghead Grisha akitokea Misri.
Hii ni mara ya tatu kwa Rais Karia kuteuliwa kuwa kamishna wa mechi zinazoendelea za fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN.
Aliteuliwa kuwa kamishna wa mechi ya ufunguzi ambapo Morocco walicheza na Mauritania Januari 13, 2018 na kisha akateuliwa tena kuwa kamishna wa mechi ya Namibia dhidi ya Zambia ambayo ilichezwa Januari 22, 2018
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...