Na Ramadhani Ali – Maelezo  .

WIZARA  ya Afya Zanzibar imetiliana saini makubaliano ya ushirikiano na Bohari ya Dawa Tanzania (msd) katika masuala ya uagiziaji dawa na vifaa Tiba kutoka viwandani moja kwa moja na hatua hiyo itaiwezesha Zanzibar kupunguza gharama kubwa ya kuagiza dawa kutoka katika makampuni.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Abdalla Juma alitia saini kwa upande wa Wizara hiyo na Mkurugenzi  Mkuu Laurean Rugambwa Bwanakunu aliiwakilishi Bohari kuu ya Dawa Tanzania katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Zanzibari Mnazimmoja.

Akizungumza baada ya kutiliana sani Bi. Asha Abdalla alisema ushirikiano huo utaisaidi Serikali na wananchi kwa jumla kuwa na uhakika wa upatikanaji dawa na kupunguza mzigo wa kutumia gharama kubwa kuagiza dawa.Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhakikisha  dawa zote zinapatikana  bila usumbufu katika Hospitali na vituo vya afya na kufanikisha  malengo yake ya kuwapatia wananchi  huduma bora za afya.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya ameshauri mashirikiano yaliyoanzishwa baina ya Bohari  Kuu ya Dawa Zanzibar na Bohari Kuu ya Tanzania yawe endelevu na kuwa mfano kwa Taasisi nyengine za pande mbili za Muungano na ukanda mzima wa Afrika Mashariki.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Abdalla Juma na Mkurugenzi Mkuu wa  Bohari ya Dawa Tanzania Laurean Lugambwa Bwanakunu wakitia saina makubaliano ya ushirikiano kati ya Wizara ya Afya  Zanzibar na Bohari Kuu ya Dawa Tanzania katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi Asha Abdalla Juma na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania Laurean Lugambwa Bwanakunu wakibadilisha hati za makubaliano baada ya kutiliana saini makubaliano hy katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania Laurean Lugambwa Bwanakunu akizungumza  baada ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano na Wizara ya Afya Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Abdalla Juma akitoa shukrani zake kwa Uongozi wa Bohari ya Dawa Tanzania  baada ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano kati yao. Picha na Abdalla Omara Maelezo - Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...