Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda jana  amezindua Jengo la Upasuaji katika Hospital ya Rufaa ya Mwananyamala yenye thamani ya zaidi ya Million 420, inayoenda kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto wakati wa kujifungua.

Jengo hilo la kisasa lenye Gorofa Moja limepewa jina la HON. PAUL MAKONDA OBSTETRIC THEATRE kama sehemu ya kuenzi jitihada za RC Makonda kuboresha Sekta ya Afya kwa kumtafuta mfadhili GSM Foundation aliekubali kujenga Jengo hilo bila kutumia pesa ya Serikali.

RC Makonda aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo hilo mnamo March 13 ,siku ambayo ndio aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa na sasa jengo limekamilika likiwa na Vyumba Viwili vya Upasuaji vyenye uwezo wa kufanya upasuaji kwa wakati mmoja na kuhudumia Wagonjwa 20 kwa siku.

RC Makonda amesema kabla ya kujengwa kwa jengo hilo Wagonjwa walikuwa wakisongamana kusubiri kufanyiwa upasuaji kitendo kilichokuwa kikisababisha Maumivu Makali na Vifo vya Mama na Mtoto, lakini kupitia jengo hilo vifo vinaenda kupungua.

Makonda ameishukuru GSM Foundation kwa kufanikisha Ujenzi wa Jengo hilo ambapo inakadiriwa Hospital ya Mwananyamala inapokea Wagonjwa kuanzia 1,500 hadi 2,000 kwa siku na Kati ya hao ni Wajawazito wanaohitaji huduma ya Upasuaji.

RC Makonda amesema hadi sasa zaidi ya Kinamama 55 wamejifungua salama ndani ya jengo hilo na linaendelea kupokea kinamama Wajawazito kila kukicha. 

Baadhi ya Kinamama waliofanyiwa upasuaji wamemshukuru RC Makonda kuwajengea jengo zuri la upasuaji linalowawezesha madaktari kufanya kazi yao pasipokuwa na usumbufu na wanafurahia kuona huduma za upasuaji zinaenda vizuri. 

Viongozi waliohudhuriwa uzinduzi huo akiwemo Mkuu wa wilaya ya kinondoni, Mstahiki Meya wa Kinondoni, watendaji wa Afya na wananchi wamempongeza RC Makonda kwa jitiada kubwa anazofanya kuboresha sekta ya Afya Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...