Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

SERIKALI ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais ,Dk.John Magufuli imeapa kutowafumbia macho viongozi au watu wanaojihusisha na shughuli za uvuvi wa kutumia zana haramu zilizopigwa marufuku.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega alipokuwa akiteketeza zana za uvuvvi haramu zilizomakatwa hivi karibuni katika Wilaya za Busega mkoani Simiyu na Magu mkoani Mwanza.

Amesema kuwa hakuna atakayesalimika katika sakata hilo endapo tu akibainika kutumia zana haramu za uvuvi.Ameongeza kuwa Serikali ina dhamira kubwa na wavuvi katka ufanyaji wa shughuli zao na ndio maana imeamua kupiga marufuku zana zote haramu kwa lengo la kusaidia kizazi kijacho ili nacho kije kinufaike na raslimali za Taifa hili.

,"Hivyo idara ya uvuvi kamwe hautomfumbia macho kiongozi yeyote yule ambaye anajishughulisha na biashara hiyo kwa kigezo cha kuwa yeye ni kiongozi.“Kwa yule atakayebainika kuwa ni kiongozi au mtu mwenye fedha zake anajihusisha na uvuvi haramu ambao Serikali inatumia fedha nyingi kukabiliana nao basi cha mtema kunde atakiona juu yake kwani zana zake zitachomwa,faini na yeye kuchukuliwa hatua za kisheria,” amesema.

Aidha Ulega amewataka wavuvi kuendelea kusalimisha zana haramu kabla ya kukumbwa na dhahma kubwa itakayowapeleka mahali pabaya zaidi ya hali ya sasa jinsi ilivyo.Pia amewahakikishia upatikanaji wa zana zinazohitajika mapema kwani tayari wamesha anza kupokea maombi mengi ya mashirika yanayohitaji kusambaza zana halali katika nchi yetu kwa madhumuni ya kuokoa rasilimali za majini zilizokuwa zikipatwa na shinda nyingi kutoka kwa wavuvui wasiokuwa waaminifu.

Kwa upande wake Msimamizi wa Kamati Maalumu ya kuthibiti na kupambana na uvuvi haramu Kanda ya Simiyu na Mwanza, Nchama Marwa amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa hakuna uonevu wa aina yeyote ile unaofanywa na kikosi hicho kuhusu kuwawajibisha wale wanaoendelea na shughuli hiyo kwa kujifisha .Ameongeza kuwa kuna wavuvi ambao wanasalimisha na wengine bado wanaendelea kuvua kwa kujifisha laniki ni lazima tu watawakamata na sheria ya uvuvi itafuata mkondo wake bila kinyongo wala uonevu wa aina yeyote ile.

Aidha kiongozi huyo wa kikosi maalumu aliwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa kazi zao kwa Naibu Waziri na kumweleza kuwa kuwa mpaka sasa wamekamata nyavu haramu za makila 33121,nyavu za dagaa175,makokoro ya sangara119.Pia nyavu za timba 3,sangara wabichi kilo 1071,sangara kayabo3463, watu hao waliokamatwa na kikosi kazi wametozwa faini kulingana na kile walichokamatwa nacho na kufikia kiasi cha Sh.milioni 767.

Naye Boniface Mkama Mkazi wa Nyamikoma wilayani Busega ameipongeza Serikali kwa kuwasaidia na vitendo vya kinyama vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya wavuvi wenzao.Hivyo ameiomba kuwawaishia tu zana sahihi ili waendelea na shughuli zao za kila siku za uvuvi.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdullah Ulega akishiriki shughuli ya kuteketeza zana haramu za uvuvvi zilizokamatwa hivi karibuni katika wilaya za Busega mkoani Simiyu na Magu mkoani Mwanza.
Mkuu wa wilaya za Busega,Tano Seif Mwera akishiriki shughuli  la kutekeza  zana haramu za  uvuvvi zilizomakatwa hivi karibuni katika wilaya za Busega mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdullah Ulega akizungumzana na wavuvi juu ya kiongozi au mtu mwenye fedha zake anajihusisha na uvuvi haramu zana zake zitateketezwa na yeye atachukuliwa hatua za kisheria.Picha na Emmanuel Massaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...