Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, ametoa agizo kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kuhakikisha wanazitambua na kuzisajili nyumba zote na viwanja vya Serikali zinazomilikiwa na Wakala huo katika maeneo mbalimbali nchini.

Agizo hilo amelitoa mkoani Mtwara, mara baada ya kukagua nyumba na viwanja vinavyomilikiwa na Wakala huo na kusisitiza kwa Mameneja wa mikoa wa Wakala huo kuhakikisha wanafanya matengenezo na ukarabati wa majengo hayo ili kuvutia wapangaji wao.

“Wasimamizi wa nyumba hizi hakikisheni nyumba hizi mnazitambua na mnazifanyia matengenezo ya mara kwa mara, nimetembelea Halmashauri mbalimbali na kuona baadhi ya nyumba za Serikali haziridhishi baada ya kuwa zimetelekezwa muda mrefu”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Aidha, Naibu Waziri huyo amemtaka Kaimu Meneja wa TBA mkoani Mtwara, kuhakikisha nyumba na viwanja vyote anavyosimamia vinakuwa na hati ili kidhibiti changamoto ya wananchi kuvamia viwanja vya Serikali.

Amekemea tabia ya baadhi ya wapangaji wa nyumba za Serikali kutozitunza wala kuzijali nyumba hizo hali inayoipelekea Serikali kuingia gharama kubwa katika kufanya marekebisho ya nyumba hizo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Mtwara Edward Mwangasa, wakati alipokuwa akikagua nyumba zinazomilikiwa na Wakala huo, mkoani humo.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Mtwara Edward Mwangasa, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, katika ukaguzi wa nyumba zinazomilikwa na Wakala huo ambao unamiliki jumla ya nyumba 76 mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, wakati alipokuwa akikagua nyumba zinazomilikiwa na Wakala wa Majengo (TBA), mkoani humo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...