Na Bashir
Yakub.
Haki ya kusajili na
kuwa na chama
cha siasa ipo
kwa kila mtanzania. Hata
wewe unaweza kuwa
na chama cha
siasa ikiwa utataka
kufanya hivyo. Wako
wanaofikiri kusajili chama
siasa ni jambo
kubwa mno. Laa hasha
ni jambo la
kawaida na utaratibu
wa usajili si
mgumu kama wengi
wanavyodhani.
Tutaona hapa utaratibu
wa kusajili chama
cha siasa. Sheria
namba 5 ya 1992
Sheria ya Vyama vya
Siasa na kanuni
zake za mwaka
1992 ndizo zinazoeleza utaratibu utakaoelezwa hapa
chini.
USAJILI HUPITIA HATUA
KUU MBILI.
Kwa mujibu
wa kifungu cha8( 1 ) cha
sheria ya vyama
vya siasa usajili
hupitia katika hatua
kuu mbili.
Kwanza usajili
wa muda na
pili usajili wa
kudumu. Kwahiyo ili
usajili chama cha
siasa yakupasa kupitia
hatua hizi mbili.
1. USAJILI WA
MUDA(PROVISIONAL REGISTRATION).
Usajili wa muda
umeelezwa katika kifungu cha
9 cha sheria
hiyo. Usajili wa
muda maana yake
chama kitasajiliwa na
kitaruhusiwa kufanya baadhi
ya kazi ila
usajili huo utakuwa
haujakamilika mpaka baada
ya kutimiza masharti, sifa na
viwango vilivyowekwa na
sheria ndani ya
muda maalum ulioainishwa na sheria. Usajili wa muda ndio unaoanza
na utaratibu wake
ni huu ;
( a ) Andaa
katiba ya chama na
hakikisha unakuwa nayo. Mnajua
kila chama cha
siasa huwa na
katiba yake, basi hiyo
ndiyo inayotakiwa hapa.
( b ) Hakikisha mko
waanzilishi wasiopungua wawili.
( c ) Andaa kanuni
za chama. Kanuni na
katiba ni tofauti. Kanuni ndizo
zinazotafsiri katiba kwahiyo kanuni
hutokana na katiba.
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...