Nteghenjwa Hosseah, Kibiti.
Wananchi wa Kata ya Mbuchi Tarafa ya Mbwera Wilayani Kibiti  mkoa wa Pwani kwa kipindi kirefu wametaabika na adha ya kukosa Daraja linalounganisha vijiji hivyo viwili vyevye wakazi zaidi ya elfu 24.
Kukosekana kwa Daraja hilo kumepelekea kukatika kwa mawasiliano ya Uhakika baina ya wananchi wa Mbuchi na wale wa upande wa Pili wa Bwera, kuongeza gharama za maisha na hata kupelekea maafa kwa wakina mama wanaojifungua na wagonjwa kwa sababu ya kukosa njia rahis na nafuu ya kuwafikisha katika huduma za Matibabu.
Vijiji hivyo ambavyo vimetengenishwa na Mto Mberambe ambao ni Tawi la Mto Rufiji na kutengeneza Delta ya Kaskazini tangu kuanzishwa kwake havijawahi kuwa na Daraja la kuwaunganisha katika shughuli zao za kila siku za kila siku za kujiletea Maendeleo.
Wananchi wa maeneo haya wamekuwa wakitumia Mitumbwi kuwavusha kutoka eneo moja hadi Lingine na huku wakitozwa Tsh 200 kwa safari moja na Pikipiki kutozwa Tsh 1000 kwa safari; Huduma hiyo hupatikana kuanzia saa kumi ba mbili asubuh hadi saa kumi na mbili jioni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng.Evarist Ndikilo na viongozi wengine wa Mkoa huo wakati wa ziara yake ya kuweka jiwe la msingi katika Daraja la Mbuchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akimpa MKandarasi maelekezo juu ya umuhimu wa daraja la Mbuchi kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu kutokana na hali adha wanayoipata wananchi wa maeneo hayo kwa hivi sasa.
Hawa ni wananchi wa kijiji cha Mbwera wakivuka kwa kutumia Mtumbwi kuja kijiji cha Mbuchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali hii ni kutokana na kukosekana kwa daraja linalounganisha vijiji hivyo lakini kwa sasa Ujenzi wa daraja hilo umeanza na utakamilika baada ya mwaka mmoja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akimskiliza Meneja wa TARURA Wilaya ya Kibiti kuhusu maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la Mbuchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...