Mamia ya Wananchi wa Wilaya za mkoa wa Ruvuma wamejitokeza kwa wingi kwenye vituo vya Usajili zoezi la Vitambulisho vya Taifa huku baadhi wakiwataka viongozi kusimamia utekelezaji wa agizo la Serikali la usajili Vitambulisho vya Taifa kuwa ni bure.

Wito huo umetolewa na wananchi wa Wilaya ya Songea wakidai kutozwa kiasi cha shs.2000/ za picha za kubandika kwenye kwenye fomu za utambulisho za Serikali za Mitaa wanakoishi na kudai gharama hizo ni kubwa kulinganisha na hali halisi ya maisha.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Mtaa wa Makambi Bwana Anuari Methodi Nyoni ametolea ufafanuzi suala hilo na kueleza wananchi wanaoagizwa kuleta picha picha ndogo za passport size ni wale ambao wamekosa viambatisho muhimu vya kuwatambulisha na hivyo ili kujiridhisha kuwa mwananchi wanayemthibitisha kuwa ni mkazi wa eneo lao basi ni vema kuwa na picha yenye taswira yake ili kuepuka matumizi mabaya ya fomu za kuwatambulisha zinazotolewa na Serikali ya Mtaa.

Aidha amesisitiza Serikali yake ya Mtaa kusimamia na kutekeleza agizo la Serikali la kwamba zoezi la Vitambulisho vya Taifa ni bure na kusisitiza umuhimu wa wananchi kuelewa Serikali inaposema zoezi ni bure haina maana kwamba Serikali itafanya kila kitu; ikutolee copy viambatisho vyako au kukulipia gharama za picha hilo haliwezekani. Amesema wao kama wasimamizi wa zoezi hilo wanasisitiza mwananchi kufika kwenye kituo na picha yake au nakala ya viambatisho vyake na huduma nyingine zote mwananchi atazifuata mtaani zinazkotolewa.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Bi. Rose Joseph amesema Mamlaka ina mashine zake za kuwapiga picha wananchi na kwamba mwananchi anayefika kusajiliwa hapaswi kuja na picha ya passport size kama inavyoelezwa; ila changamoto kubwa ni kwa wale wananchi ambao hawana viambatisho vyovyote vya kuwatambulisha na wanahitaji kupata barua ya utambulisho wa Serikali za Mitaa wanakoishi. 
Wananchi wakazi wa Kata ya Ndilima Mtaa wa Makambi Ndilima Wilaya ya Songea, wakikagua fomu zao kabla ya kwenda kwenye maalumu cha uchukuaji taarifa kwa maana ya kupigwa picha, uchuaji alama za kibaiolojia na saini ya Kielekrtoniki. Waliopo pichani ni Bi. Hadija Yahaya (mwenye gauni la Pinki kushoto) na Bwana Hussein Nyoni (Mwenye kofia kichwani) wote wakazi wa Mtaa wa Makambi Songea. 
Hawa ni baadhi tu ya wakazi wa Kata ya Ndilima Wilaya ya Songea wakisubiri huduma ya Usajili Vitambulisho vya Taifa unaoendelea kwenye shule ya msingi ya Matogo na kuhusisha wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea. Kwa Wilaya ya Songea Kata zilizoanza zoezi ni Kata ya Ndilima na Seed-farm zoezi ambalo litafanyika wa siku saba tu kabla ya kuhamia Kata zingine za Wilaya hiyio.

Akionekana mwenye furaha ni Bi Haruna Thabiti Majwila wa Mtaa wa Makambi Ndilima mara baada ya kukamilisha hatua za usajili kwa maana kupigwa picha na kuchukuliwa alama za Kibaiolojia. Na hapa ya akiangalia muonekano wa Kitambulisho chake utakavyokua na kukagua picha yake kujiridhisha endapo picha yake imetoka vizuri. Kulia ni Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bwana Agaton Magnus Komba. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...