- Mkandarasi asiyeanza kazi ifikapo Machi 2 kukiona cha moto
- Viongozi TANESCO, REA wawasilishe taarifa kila robo mwaka
Na Veronica Simba – Dodoma.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amekutana na watendaji mbalimbali wanaosimamia na wanaotekeleza miradi ya awamu ya tatu ya kusambaza umeme vijijini na kutoa maagizo mazito yanayolenga kufanikisha mradi huo kikamilifu.
Mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa Juma, Januari 13 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, ulihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri Kalemani alitoa maagizo kwa wajumbe ambao ni wazalishaji na wasambazaji wa nguzo, transfoma na nyaya za umeme, wakandarasi wanaotekeleza mradi husika katika maeneo mbalimbali nchini na wataalam wanaosimamia utekelezaji wa mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA); kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ipasavyo.
Kwa upande wa wakandarasi, Dkt. Kalemani aliwaagiza kuhakikisha kila mmoja anaanza utekelezaji wa kazi halisi (physical work) kabla ya tarehe 2 Machi mwaka huu vinginevyo Serikali itawachukulia hatua za kisheria. “Asiwepo mkandarasi yeyote ambaye atakuwa hajaanza kazi baada ya tarehe hiyo, alisisitiza.”
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akisisitiza jambo wakati
akiongoza kikao baina yake na wadau mbalimbali wanaotekeleza miradi ya
usambazaji umeme vijijini awamu ya tatu. Kushoto ni Naibu Waziri wa
Nishati, Subira Mgalu na kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Haji
Janabi.
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (aliyesimama) akizungumza wakati wa
Mkutano na wadau mbalimbali wanaotekeleza miradi ya usambazaji umeme
vijijini awamu ya tatu. Kushoto kwake ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani.
Wakandarasi
mbalimbali wanaotekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijini awamu ya
tatu, wakielezea hatua waliyofikia katika utekelezaji wake katika kikao
baina yao na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Dodoma mwishoni mwa
Juma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...