Na Greyson Mwase, Dar
es Salaam.
Zabuni kwa ajili ya
mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme wa Megawati 2100 la Steigler's Gorge katika Maporomoko
ya Maji ya Mto Rufiji zimefunguliwa leo
tarehe 02 Februari, 2018.
Akizungumza wakati wa
ufunguzi wa zabuni hizo kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar
es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi kutoka Wizara ya Nishati, Amon
MacAchayo amesema zabuni hizo ni za Awamu ya Pili kutokana na kukosekana kwa
mshindi katika Awamu ya Kwanza iliyotangazwa mapema mwaka jana.
Alisema
kuwa, katika awamu ya kwanza jumla ya kampuni 81 zilinunua nyaraka za zabuni
ambapo nakala moja ilikuwa inauzwa kwa shilingi 200,000 lakini ni kampuni nne
tu zilifanikiwa kurejesha maombi na kuongeza kuwa kampuni zote nne hazikuwa
na vigezo vinavyohitajika hali
iliyopelekea kutangazwa upya kwa zabuni tarehe 19 Desemba, 2017 katika vyombo
vya habari vya ndani na nje ya nchi.
MacAchayo
aliongeza kuwa, katika awamu ya pili kampuni 17 zilijitokeza katika ununuzi wa
nyaraka kwa gharama ya shilingi 500,000 kwa kila moja ambapo mpaka siku
zinafunguliwa ni kampuni tano tu zimerejesha nyaraka zenye maombi ya zabuni.
Alisema
hatua inayofanyika kwa sasa ni ufanyaji wa tathmini ya zabuni hizo na
kusisitiza kuwa mara baada ya kukamilika kwa tathmini ya zabuni hizo waombaji
wote watajulishwa mshindi na baada ya hapo zitafuata taratibu za mazungumzo,
barua na kuandaa mkataba kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi mara moja.Aliwataka
kampuni zilizowasilisha maombi kuwa watulivu wakati zoezi la tathmini
likiendelea.
Mkurugenzi
wa Idara ya Manunuzi kutoka Wizara ya Nishati, Amon MacAchayo (mbele)
akizungumza na wawakilishi wa kampuni mbalimbali zilizoomba zabuni kwa ajili ya
mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme katika Maporomoko ya Maji ya Mto
Rufiji kwenye ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam tarehe 02
Februari, 2018
Mtaalam
wa Manunuzi kutoka Wizara ya Nishati, Jackson William (kulia) akieleza jambo
kwenye ufunguzi huo. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi kutoka Wizara
ya Nishati, Amon MacAchayo na aliyekaa kushoto ni mwakilishi wa kampuni
zilizoomba zabuni, Khaled Makkawy kutoka
kampuni ya The Arab Contractors
Sehemu
ya wajumbe wakifuatilia zoezi la ufunguaji wa zabuni kwa ajili ya mradi wa
Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme katika Maporomoko ya Maji ya Mto Rufiji
katika kikao hicho.
Wataalam
kutoka Idara ya Manunuzi, Wizara ya Nishati wakifungua nyaraka mbalimbali za
zabuni katika kikao hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...