Na Agness Francis, Globu ya Jamii
MABINGWA wa Afrika Mashariki na Kati Azam Fc wanatarajia kushuka dimbani kesho kuumana na Wanakuchere NdandaFc katika mchezo wao wa marudiao raundi ya pili, Ligi kuu Tanzania Bara utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari AzamFc Jaffary Iddy Maganga, amesema katika mtanange huo utakaoanza saa 10 jioni, kikosi chake kitawakosa wachezaji wake mahiri 5.
Amewataja wachezaji hao ni Himidi Mau, Waziri Junior, Joseph Mahundi, Joseph Kimwaga na Aboubakar Salum maarufu kama (Sure Boy) anayetumikia adhabu ya kadi Nyekundu aliyoipata wakati wa mechi dhidi ya Mabingwa watetezi Tanzania Bara Yanga SC.
"Licha ya kuwakosa wachezaji hao, tuko vizuri na kikosi chetu ni kipana chenye uwezo mkubwa, tutahakikisha tunapambana vikali dhidi ya Wanakuchere ili tunachukue pointi 3,"amesema Jaffary Maganga.
Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Azam Fc Aristica Cioaba amesema kuwa wamejiandaa vema kwa mchezo huo kiakili, kimwili huku akitamba kuwa kikosi chake kiko kwenye mazingira mazuri.
Afisa Habari AzamFc, Jaffary Iddy Maganga akizungumza na waandishi wa habari katika kuelekea Mtanange wa patashika nguo kuchanika pale Uwanja wa Azam Complex Chamazi wakiwa wenyeji wa NdandaFc katika kuuchapa mchezo wao wa Marudiao raundi ya 2 Ligi kuu Tanzania Bara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...