Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Marehemu Kingunge Ngombale Mwiru kufuatia kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 2 Februari 2018, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, natoa pole kwa familia ya  marehemu na Watanzania kwa ujumla kwa kumpoteza mwanasiasa Mkongwe katika nchi hii ambaye licha ya kuwahi kuwa Mbunge lakini pia ameitumikia Serikali katika nyadhifa mbalimbali,” alisema.

“Binafsi nilifanya kazi kwa karibu na Mzee Kingunge wakati wa Bunge letu na pia kwenye Bunge la Katiba ambapo tulikuwa wote kamati namba nane nikiwa Mwenyekiti wake, mchango wake ulitusaidia sana” aliongeza Mheshimiwa  Spika.

Mheshimiwa Spika amemuomba Mwenyezi Mungu awape subira, nguvu na faraja familia, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kupotelewa na mpendwa wao.

 Imetolewa na:      Ofisi ya Spika
S.L.P. 941

DODOMA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...