Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) ,Said Sudi Said amesema chama kimejipanga kushika dola katika uchaguzi  mkuu utakaofanyika mwaka 2020 kutokana na mikakati walioiweka ya kushika dola hiyo.
Said  ambaye ni Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar aliyasema hayo katika Uchaguzi Mkuu chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa Executive  jijini Dar es Salaam, amesema kuwa AFP ni chama chenye mtazamo chanya katika masuala ya uongozi ya kuwatumikia wananchi.
Amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imeweza kuleta amani kwa wananchi lakini wenyewe wakishika dola watafanya zaidi kudumisha amani.
Nae Katibu Mkuu wa Chama hicho, Rashidi  Rai amesema kuwa wabunge waangalie sheria ya uchaguzi mdogo kuwa imebadilishwe kwa mtu atakayejiuzulu uchaguzi usifanyike badala yake Mbunge wa jimbo lilokaribu ataweza kutumikia.
Amesema kuwa ni gharama kubwa ya uchaguzi kwa fedha hizo zinaweza kutumika katika masuala mengine ya maendeleo ya wananchi kutokana na changamoto zilizopo za kukosekana kwa fedha.
Katika uchaguzi Mkuu Said Sudi Said alishinda nafasi hiyo kwa kura zote za wajumbe wa mkutano mkuu pamoja na Katibu Mkuu huku na nafasi zingine za jumuiya zilishapata  viongozi
 Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) , Said Sudi Said akizungumza katika mkutano mkuu wa chama hicho pamoja na uchaguzi mkuu uliofanyika katika katika ukumbi wa Executive jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Chama cha AFP, Rashidi Rai akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu kuhusiana na utaratibu wa uchaguzi mkuu uliofanyika katika ukumbi wa Executive jijini Dar es Salaam. 
 Wajumbe wa Mkutano mkuu wa Chama cha AFP.
Sehemu ya Wasimamizi wa uchaguzi Mkuu wa Chama cha AFP.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...