Na Ripota Wetu,Globu ya Jamii
MKUU wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Sophia Mjema , amemuagiza Mwwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Kata ya Liwiti Salima Fumbwe kuandaa vijana na wanawake wa kata hiyo kwa lengo la kupatiwa elimu ya uchukuaji wa mikopo ya Serikali na kisha kuirejesha.
Akizungumza juzi wakati amekutana na wananchi wa kata ya Liwiti wilayani humo, Mjema ameelezea umuhimu wa vijana na wanawake kupata elimu inayohusu mikopo inayotolewa na Serikali na kisha kuirejesha ili wengine nao wakope.
" Salima kama kiongozi wa wanawake wa kata hii uje ofisini kwangu nikupatie maofisa maendeleo waje kutoa elimu ili vijana wapate fursa hiyo ya kupata mikopo ya Serikali.Muda wowote njoo pale ofisini,"DC Mjema amemueleza mwenyekiti huyo wa UWT.
Amesema fedha hiyo ya Serikali mara baada kuipata wakumbuke marejesho na kueleza wachukue mikopo hiyo na kuitumia kwa malengo maalum.Mjema amesema taratibu zote watapewa kupitia ofisi ya Ofisa Mtendaji wa Kata ya Liwiti kupitia maofisa maendeleo wa kata.
Pia amemuagiza Mwenyekiti huyo wa UWT kuweka utaratibu wa vijana wake ili kupata fursa hiyo kata ya Liwiti.Ameongeza anajua wapo vijana wengi wanashindwa kujishughulisha kutokana na kukosa mitaji,hivyo mikopo hiyo itawasaidia katika shughuli za ujasiriamali .
Kwa upande wake Fumbwe amempongeza Mjema aliyekuwa mgeni rasmi kuwa atahakikisha anafuatilia na kutekeleza maagizo ya Serikali."Tutaweka mpango maalum vijana na wanawake wote wa Liwiti waweze kuwa na fursa ya kukopa." Nitashirikiana na wanachama wenzangu na Katibu wangu wa UWT kuweka mazingira bora kwa wanawake wote,"amesema.
Amefafanua yeye kama kiongozi wa UWT msimamo wake ni kwamba wanawake wote wajikwamue kiuchumi ili wasiwe tegemezi .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...