Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dkt. Mwigulu Nchemba akizindua zoezi la uandikishaji wa wananchi kupata kitambulisho cha uraia mkoani Tabora kushoto kwake ni kaimu mkurugenzi mkuu wa NIDA Andrew Masawe na mkuu wa wilaya ya Tabora Queen Mlonzi. zoezi hilo lilifanyika leo katika wilaya ya Tabora
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka watanzania kujiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa kwani si zoezi la hiari ni lazima kwa mtanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi ili kutambukiwa.
Waziri Mwigulu amewataka wananchi waache mazoea ya kutafuta kutambuliwa mpaka wanapokuwa na shida hasa za kutaka hati ya kusafiria au migogoro ya ardhi pale anapoambiwa yeye si raia wa Tanzania .
“Zoezi hili ni bure kujiandikisha na kupata kitambulisho pasitokee kiongozi yeyote wa wilaya na vijiji kuchangisha fedha wananchi ili wapate fomuza kujiandikisha na wala zoezi hili lisiunganishwe na siasa.”alisema Dkt.Mwigulu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...