Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Canine Association Ltd (TCAL) Sinare Sinare, akizungumz na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, leo wakati akitangaza uzinduzi rasmi wa Chama cha Wamiliki wa Mbwa utakaofanyika katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni siku ya jumamosi,Januri 3,2018. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Inspector General wa Polisi (IGP) Simon Siro. Kushoto kwake ni Wajumbe wa Kamati ya uzinduzi huo, Felicia Bulu na Deo Rweyunga. (kushoto) ni Kamanda wa Polisi Kikosi cha Mbwa na Farasi, Dkt. Egyne Emmanuel. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO).
Mkutano ukiendelea.
Na Amina Kasheba, Dar (DSJ)
MKURUGENZI
wa Kampuni ya Tanzania Acanine Association Limited(TCAL),Dk. Sinare
Sinare amesema Februari 3 mwaka huu wanatarajia kuzindua rasmi Chama cha
Mbwa nchini ambapo mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo atakuwa Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo, Dk.Sinare amesema lengo la kuanzishwa kwa
chama hicho ni kuwakutanisha wadau na wamiliki wa mbwa nchini ili
wajenge ushirikiano miongoni mwao.
"Tunaomba
wadau wote wakiwamo wanaofuga na wasiofuga mbwa tukajumuika
pamoja.Pamoja na mambo mengine kwa kutumia chama hiki pia tutakuwa na
kazi ya kusimamia na kushauri kuhusu uzalishaji wa mbwa bora,"amesema
Dk.Sinare.
Ameongeza wanataka kuona wamiliki wa
mbwa na wadau wote wanakuwa na sauti ya pamoja na siku ya uzinduzi
hakutakuwa na kiingilio, mtu yoyote ataruhusiwa kuhudhuria na kujionea
michezo ya Mbwa na Farasi,"amesema.
Akielezea
zaidi kuhusu uzinduzi huo, Dk.Sinare amesema Kikosi cha Mbwa cha Polisi
nacho kitaonesha uwezo wa mbwa wao katika kulinda usalama wa raia na
mali zao.
"Baada ya kuzindua chama hicho
tutaanza maandalizi ya kuandaa maonesho makubwa ya mbwa yatakayofanyika
Juni 6 mwaka huu na nchi mbalimbali kutoka Barani Afrika watashiriki
maonesho hayo,"amesema Dk.Sinare.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...