Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango  akiwa katika Picha ya Pamoja  Ofisini kwake baada ya kutembelewa na Naibu Kamishina wa Polisi DCP Ahmada.A. Khamis Mkuu wa Kitengo  cha Polisi Jamii, Mkuu wa Kituo cha Polisi Nachingwea, SP Kasigwa, na Meneja Mwandamizi wa huduma za Uwakala Benki ya CRDB  Bwa.Donath Mushi, Wengine ni Abel Laswai  meneja mauzo wa wateja wadogo (wa kwanza kushoto) na Inspekta Issa Asali kutoka kitengo cha Polisi Jamii (wa mwisho kulia). Jeshi la Polisi pamoja na maafisa wa Benki ya CRDB  kutoka Makao Makuu Dar es salaam wapo Mkoani Lindi kwa ajili  kutoa elimu kwa umma juu Matumizi salama ya huduma za ki benk pamoja na elimu juu ya wizi wa fedha kwa njia ya mtandao.
 Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango akimkabidhi zawadi ya Korosho  kwa niaba ya wananchi wa wilaya hiyo Naibu Kamishina wa  Polisi DCP Ahmada.A.Khamis. Zawadi hiyo ilitolewa kama shukrani na wananchi  wa wilaya hiyo kutokana na elimu waliyopewa.
Meneja Mwandamizi wa huduma za uwakala kwa Benki ya CRDB Donath Mushi akitoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Naipingu iliyopo wilayani Nachingwea Mkoani Lindi, Jana juu ya matumizi salama ya Huduma za bank ma uhifadhi salama wa fedha katika benki hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...