Mkuu wa Kitengo cha Uchumi
na Takwimu Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (ACF) Maria
Kullaya amepokea msaada wa Kompyuta mpakato moja na Printa moja kutoka katika
Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.Ltd, kwa ajili ya kuboresha kitengo cha
Takwimu cha Jeshi hilo.
Msaada huo wenye thamani ya
sh.1.5 million ambao umetolewa na Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.Ltd
umepokelewa mapema leo Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliopo barabara ya Ohio
Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati akipokea
msaada huo Kamishna Msaidizi Maria alisema, msaada huu umetolewa wakati muafaka
kwani utasaidia kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi katika ukusanyaji wa
taarifa na utunzaji wa kumbukumbu tofauti na hapo awali.Tunatarajia kuvitumia vifaa
hivi kwa lengo mahususi pamoja na kuvitunza vizuri “Vifaa hivi vitakuwa chachu
kwa kitengo cha takwimu kwani tulikuwa na uhaba wa vitendea kazi” alisema
Kamishna Msaidizi Maria.
Naye Meneja wa Kampuni hiyo
Bw. Rigobert Massawe, akizungumza wakati akikabidhi msaada huo, alisema “lengo
ni kuliwezesha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutimiza majukumu yake kwa ufanisi
kwani kwa kufanya hivyo tunatimiza wajibu wetu wa kurudisha huduma kwa jamii”.
Kamishna Msaidizi Maria
anaishukuru kampuni hiyo kwa kuwapa msaada wa vitendea kazi hivyo, pia kupitia
nafasi hii naomba wadau wengine waige mfano huu kwa kulisaidia Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji katika Nyanja mbalimbali ili liweze kutimiza majukumu yake ya kuokoa
Maisha na Mali za Watanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Takwimu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Msaidizi (ACF) Maria Kullaya (kulia) akipokea msaada wa Kompyuta mpakato na Printa kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.ltd Bw. Rigobert Massawe (kushoto). Vifaa vitakavyosaidia kutunza kumbukumbu za takwimu za majanga mbalimbali yanayotokea nchini, msaada huo umepokelewa Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo.
Meneja wa Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.ltd Bw. Rigobert Massawe (kushoto) akimkabidhi Kompyuta mpakato (Laptop) Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Takwimu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Msaidizi (ACF) Maria Kullaya (kulia) (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji).
Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Takwimu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Msaidizi (ACF) Maria Kullaya wa nne kutoka (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.ltd Bw. Rigobert Massawe wa tano kutoka (kulia), Meneja rasilimali watu wa Kampuni hiyo Bw. Danial Mbonea wa tatu kutoka (kulia) na Maafisa wa Jeshi hilo wakati wa makabidhiano ya msaada wa Komputa mpakato na Printa, mapema leo Makao Makuu ya Jeshi hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...