Na Said Mwishehe, Blogu ya jamii
KADA mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi ameeleza sababu zinazochangia kudhoofika kwa vyama vya upinzani nchini.
Amesema
kuyumba kwa vyama hivyo kunachangiwa na ubinafsi waviongozi wake ambao
wengine wageuza Chama ni mali yao na kutoamaamuzi ambayo si shirikishi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,Katambi
amesema kuwa tanguameondoka Chadema ambako alikuwa Mwenyekiti wa Vijana
na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho amekuwa kimya muda mrefulakini
ameona ni vema akasema mambo kadhaa kuhusu hali ya kisiasa nchini.
Kuhusu
vyama vya siasa kuyumba, Katambi amesema zipo sababuambazo zimekuwa
zikichangia vyama hivyo kushindwa kuwa imara namatokeo yake kubaki
kulalamikia kila jambo ambalo linafanywa naSerikali hata liwe lenye
maslahi kwa nchi.
"Upinzani
umeshindwa kujenga chama taasisi kwani hivi sasa kilachama ni cha
mtu.vyama vingi ni vya watu na si taasisi.Dhana yataasisi ni kwamba
sheria ,kanuni na taratibu lazima zifuatwe"Kama mtu anadharau katiba na
misingi iliyowekwa basi huo niudikteta. Wapinzani kabla ya kukimbilia
kugombea udiwani na ubunge wajikite kwanza kujenga taasisi, kama
wameshindwa kuheshimu katiba za vyama vyao wanapate uhalali wa kudai
Katiba,"amesema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...