Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

WIMBI la baadhi ya viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) limezidi kuwakumba hapa nchini baada ya katibu wa CHADEMA kata ya MailMoja Mjini Kibaha Mohamed Hashim kuhamia CCM.

Pamoja na hayo wanachama wengine wa CHADEMA na ACT Wazalendo wapatao tisa nao walirejea CCM na kukabidhi kadi zao kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ramadhan Maneno.

Hayo yalijiri Kongowe wilayani Kibaha wakati Maneno alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa wilayani humo.Maneno alisema, kwa sasa wapinzani wameshatambua vyama hivyo kuwa hakuna jipya hivyo wameamua kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli ambaye anatatua kero na changamoto zilizokuwa zinawasumbua wananchi.

“Hichi ndicho kielelezo cha kumkubali kiongozi wetu wao wenyewe wameona kinachofanyika na kasi na mabadiliko ya kimaendeleo iliyopo,” alisema Maneno.Alisema kuwa wanaCCM wanapaswa kukiimarisha chama kwa kuhakikisha wanalipa ada zao kwa wakati kwani ili mwanachama awe hai lazima alipe ada zake .

“Tunawanachama 38,000 kwenye Mji wa Kibaha lakini waliolipa ada ni wanachama 8,000 pekee ,,:;si sawa lazima wanachama watakeleze jukumu lao hilo ili kujenga chama,” alisisitiza Maneno.Alielezea kwa sasa viongozi waendelee kuhamasisha wananchi kujiunga CCM kwani mtaji wa chama ni kuongeza wanachama wapya.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani, Ramadhani Maneno akizungumza jambo na baadhi ya  viongozi ,wa CCM Mjini Kibaha na halmashauri ya mjini hapo wakati wa ziara yake mjini humo .
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani, Ramadhani Maneno akisalimiana na  baadhi ya  viongozi ,wa CCM Kata ya Kongowe na Mjini Kibaha kabla ya mkutano nao ,kuzungumzia masuala mbalimbali ya Chama wakati wa ziara yake mjini humo .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani, Ramadhani Maneno akipokea kadi kutoka kwa katibu wa CHADEMA kata ya MailMoja Mohamed Hashim aliehamia CCM wakati mwenyekiti huyo alipokuwa akizungumza na baadhi ya wanachama na viongozi ,katika mkutano huo wanachama wengine Tisa kutoka upinzani walijiunga na Chama hicho.(picha na Mwamvua Mwinyi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...