Kongamano
la kumi la Fema Clubs kutoka kote nchini limemalizika leo jijini Dar es
Salaam likiwa limekutanisha wanafunzi zaidi ya mia moja pamoja na
walimu wao. Hawa ni wawakilishi kutoka mikoa yote ya Tanzania.
Hili ni tukio ambalo shirika la Femina Hip hulifanya kila mwaka kama sehemu ya kuwaongezea uwezo vijana wanachama wa Clubs za Fema na pia walimu wao walezi, katika kutekeleza azma ya kuleta mabadiliko ya tabia na kujenga kizazi kinachozingatia mitindo bora ya maisha.
Kila mwaka kongamano huongozwa na mada maalum, na kwa mwaka huu kauli mbiu ni Ukatili wa Kijinsia Sasa Basi. Kauli mbiu hii inaakisi mkazo unaowekwa na shirika pamoja na wadau wake kupambana na matukio na tabia ambazo huwaumiza watu kwa sababu ya jinsi zao.

Toleo jipya la jarida la Fema
limesheheni simulizi za kweli na uzoefu wa watu ambao ama walifanya
ukatili au walifanyiwa, lakini sasa wanasimama na kutuhimiza sote
kuukataa ukatili wa kijinsia. Toleo hili lilizalishwa pamoja na wadau
mbalimbali ikiwemo UNICEF, CDF na Plan International, na kama anavyosema
Mkurugenzi Mkuu wa Femina Hip, Dr Minou Fuglesang, “Juhudi zetu hizi ni
sambamba na juhudi za serikali kutokomeza ukatili dhidi ya wananawake
na watoto kama zilivyoainishwa katika mpango wa kitaifa uliozinduliwa
mwaka jana.”
Mafunzo na mijadala ambayo ilifanyika wakati wa kongamano hili ililenga kuwaandaa wana Fema Club kuwa vinara wa mabadiliko, kuongoza mchakato muhimu wa kuelimisha jamii zao na kuhamasisha tabia zinazopingana na ukatili huu.
Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig akikabidhi zawadi kwa mwalimu Kahwa Mpunami wa Misungwi High ambao wameshinda (BEST FEMA CLUB OF THE YEAR 2017) Klabu Bora ya mwaka 2017 kutoka shule ya sekondari ya Myunzi Korogwe Tanga baada ya kutangazwa mshindi katika kipengele hicho katika kongamano la kujadili namna ya kupunguza ukatili wa Kijinsia kwa watoto wa kike likiwa na kauli mbiu ya "Ukatili wa Kijinsia sasa BASI" na kushirikisha Klabu mbalimbali za FEMA kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania , Kongamano limemalizika leo na lilikuwa likifanyika kwenye hoteli ya Seascape Mbezi Beach jijini Dar es salaam kwa siku nne mfurulizo, Kongamano hilo limehusisha pia mafunzo ya mambo mbalimbali. , Katika picha anayeshuhudia ni Dr. Minou Fuglesang Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Femina Hip Tanzania.
Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig akikabidhi zawadi kwa Mayombo Lutego ambaye ameshinda (BEST FEMA CLUB MENTOR OF THE YEAR 2017) .kutoka shule ya Sekondari ya Misungwi mkoani Mwanza baada ya kutangazwa mshindi katika kipengele hicho katika anayeshuhudia ni Dr. Minou Fuglesang Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Femina Hip Tanzania.
Upendo Abisai kutokamwanachama wa Youth For Change Project uliopo chini ya Plan International Tanzania akitoa mada katika kongamano hilo kutoka kushoto ni watoa mada wengine Lydia Charles Mtangazaji wa Kipindi cha Fema TV Show na Fema Radio Show, Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig, Amabilis Batamula Mkurugenzi wa Habari Femina Hip na Koshuma Mtengeti Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Childrens Dignity Forum (CDF)

Baadhi ya wanafunzi shule mbalimbali za sekondari nchini kutoka klabu za Fema Hip wakifuatilia mada katika kongamano hilo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...