Ni mwaka moja umepita tokea ulipotuacha. Tokea ulipotoweka hakuna siku inayopita ambapo haupo katika mioyo na akili zetu. Enzi za uzima wako matendo yako yaligusa mioyo mingi kwa namna ya kipekee ambayo Wewe tu uliweza. 

Roho yako ya huruma bado ipo pamoja nasi na mara kwa mara hugusa mioyo na akili zetu na kutupa sababu ya kutabasamu. Umejitwalia nafasi yako miongoni mwa nyota za mbinguni na shime ung’ae milele. Unakumbukwa sana na kila mtu hapa duniani. Ulitoweka kwa uchungu sana bila  hata ya kutuaga. 

Tunakufikiria sana kimyakimya. Hakuna jicho linaloweza kutushuhudia tukiomboleza, ila machozi mengi yanatiririka ndani kwa ndani. Tunafarijika kwa kutambua kuwa ipo siku tutakutana na Wewe tena. Unakumbukwa sana na watoto, wakwe na wajukuu wako.

Familia ya Marehemu Balozi Cecil A Kallaghe inawaalika ndugu na marafiki wote katika Misa ya Kumbukumbu tarehe 3 Februari 2018 itakayofanyika katika kanisa Kuu la Anglikana la Mtakatifu Albano Dar es Salaam saa 2 asubuhi. Mkesha utafanyika nyumbani Mbezi Temboni tarehe 2 Februari 2018. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...