Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachiwa huru mfanyabiashara Abdullah Hauga (73) aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa kupeperusha bendera ya Tanzania bila kibali.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Nolle Prosequi kuwasilisha chini ya kifungu cha sheria namba 91(1) cha mwenenendo wa makosa ya jinai kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya Hauga.

Kabla ya kuachiwa, Mahakama ilitupilia mbali hati ya kuzuia ya dhamana ya DPP na  kisha kutoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa.Mbali ya Hauga mshtakiwa mwingine ni Mkurugenzi wa Meli ya Lucky Shipping, Issa Haji (39).

Mapema, Wakili wa Serikali, Salim Msemo alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa kwamba shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya uamuzi kuhusu DPP kuzuia dhamana kwa washtakiwa.Katika uamuzi wake, Hakimu Nongwa amesema alisikiliza hoja za pande zote mbili na pia amesoma uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ambayo imemuondolea DPP mamlaka ya kuzuia dhamana.

Hakimu Nongwa amesema Mahakama ya Rufaa ndio ya juu nchini, hivyo maamuzi yake lazima yaheshimiwe kwani kuzuia dhamana kwa washtakiwa ni kuwanyima haki.Amesema kibali cha DPP kimewasilishwa wakati Mahakama ya Rufaa nayo imetoa uamuzi kuhusu suala hilo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...