Mwishoni
mwa wiki Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametembelea na kukagua
utekelezaji wa Miradi ya umeme vijijini (REA II & REA III)
kwenye jumla ya vijiji 18 katika wilaya za ROMBO, MWANGA NA SAME Mkoani
Kilimanjaro.
Katika
ziara hiyo Naibu Waziri aliongea na wananchi, pia kutambulisha
wakandarasi wa miradi ambapo aliwaagiza wakandarasi waepuke kurudia
makosa yaliyojitokeza awali na kuhakikisha wanakamilisha kazi ndani ya
muda uliopangwa.
Pia
Katika ziara hiyo Mh. Naibu waziri alitembelea bwawa la kuzalisha umeme
la NYUMBA YA MUNGU kujionea shughuli za uzalishaji.Naibu waziri
amemaliza ziara yake Januari 26/2018 na kuelekea jijini TANGA.
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwaeleza wananchi wa kijiji cha
Mkisha kuhusu kifaa kijulikanacho kama UMETA (REDY BODY) kifaa hicho
hutumika kama mbadala wa kusuka mifumo ya waya (wiring) ndani ya nyumba.
Aliyeshika kifaa hicho ni Afisa uhusiano TANESCO KILIMANJARO Bw.
Samuel Mandari.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wanakijiji na kueleza uhitaji wa huduma ya umeme.
Wanakijiji wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) akieleza uhitaji wa huduma ya umeme.
Mh.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Mkuu wa wilaya ya Same Mh.
Rosemary Senyamule, Kamati ya Ulinzi na usalama wilaya, wakiwa na
viongozi wa TANESCO MKOA wa Kilimanjaro walipo tembelea Kijiji cha Vunta
wilayani Same.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...