Na Dixon Busagaga,Moshi.
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania ,Kanda ya Moshi ,imemuhukumu kifungo cha maisha jela ,Christina Biskasevskaja (26) raia wa nchi ya Lithuania baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin na Hydrochloride kinyume cha sheria .
Hukumu hiyo imetolewa jana Mahakama kuu ya Tanzania ,Kanda ya Moshi na Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu ,Aishieri Sumari ambapo upande wa utetezi ulikuwa ukiwakilishwa na Mawakili Patrick Paul na Gwakisa Sambo huku upande wa jamhuri ukiwakilishwa na Jopo la Wanasheria wa serikali wakiongozwa na Tamari Mndeme .
Akisoma hukumu ,Jaji Sumari alieleza kuwa mahakama imejiridhisha kupitia ushahidi usio na shaka uliowasilishwa na mashahidi wapatao saba wa upande wa Jamhuri unlimtia hatiani mshtakiwa huyo ambao ulieleza kukutwa na Dawa hizo zikiwa na uzito wa gramu 3775.26 na thamani ya sh za kitanzania Mil 169,886,700.
Biskasevskaja ambaye pia anatajwa kuwa msanii wa Muziki alikamatwa Agosti ,28 mwaka 2012 majira ya saa 9:16 za mchana katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) wakati akijiandaa kuelekea katika mji wa Brussels Ubelgiji kupitia Addis Ababa Ethiopia.
Christina Biskasevskaja (26) raia wa nchi ya Lithuania akiwa chini ya Ulinizi baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin na Hydrochloride kinyume cha sheria .





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...