Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira akitoa maelekezo kwa Meneja wa
Tanesco Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka, pembeni ni Mhandisi mkuu wa
mkoa Bagabuje Joseph, Mkuu wa wilaya ya Moshi Mh. Kippi Warioba na
Meneja wa Tanesco Himo, Bw, Mohamed Kayanda.
Mhandisi
usafirishaji mkoa wa Kilimanjaro Yared Ngalaba akifafanua kwa Mkuu wa
mkoa Mh Anna Mghwira mifumo ya usafirishaji umeme mkoani Kilimanjaro.
Kutoka
kushoto Mhandisi usafirishaji mkoa wa Kilimanjaro Yaredi Ngalaba,
Mhandisi mkuu Bagabuje Joseph, Afisa uhusiano Tanesco Kilimanjaro Bw.
Samuel Mandari na Meneja wa Tanesco Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira.
Msimamizi wa kituo cha kupoza umeme cha Kiyungi Joseph Mwisongo akifafanua jambo kwa Mkuu wa mkoa Mh Anna Mghwira.
- KATIKA ZIARA HIYO AMETEMBELEA VITUO VYA KUPOOZA UMEME (SUBSTATIONS) ZA KIYUNGI, TRADE SCHOOL, BOMA MBUZI NA KIA.
Mkuu
wa Mkoa Amewataka watumishi wa TANESCO kuendelea Kutekeleza majukumu
yao kwa bidii ili kuhakikisha huduma ya umeme inakuwepo muda wote na
ameahidi kuwaunga mkono katika ulinzi wa miundombinu ya umeme mkoani
hapa.
Nae
meneja wa TANESCO Kilimanjaro mhandisi MAHAWA MKAKA amemuhakikishia
Mkuu wa mkoa kuwepo kwa umeme wa kutosha kwa wawekezaji wa viwanda
Mkoani Kilimanjaro.
Katika
Ziara hiyo Mkuu wa mkoa aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa pamoja na
wakuu wa wilaya za Moshi na Hai pamoja na viongozi mbalimbali wa
Serikali Mkoa na Wilaya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...