Na Stella Kalinga

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesitisha malipo ya shilingi bilioni 1.9 kwa wakandarasi watatu, ambao ni Simiyu Investiment Co. Ltd, Nselema Associtates Co. Ltd na Great Lakes Construction Co.LTD, wanaotekeleza miradi saba ya maji wilayani MEATU ambayo imeshindwa kukamilika tangu mwaka 2014.

Agizo hilo amelitoa wilayani Meatu, mara baada ya kukagua miradi ya maji ya Lubiga, Itinje na Bukundi na kutoridhishwa na kazi iliyofanyika.

“Tunasitisha malipo yote ya wakandarasi watatu wanatekeleza miradi saba ya maji ndani ya Wilaya ya Meatu, malipo yafanyike baada ya Wataalam wetu wanasheria, wahandisi wa maji wa Halmashauri ya Meatu, Mhandisi wa Maji Mkoa, Mwanasheria ya Mkoa na timu ya Mkoa kujiridhisha; ikiwa wanastahili kulipwa watalipwa ikibainika hawana sifa tunavunja mkataba” alisisitiza Mtaka.

Pamoja na kusitisha malipo hayo Mtaka amesema makampuni hayo hayataruhusiwa kufanya kazi za ukandarasi katika miradi yoyote wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthoy Mtaka(kulia) akiwa na baadhi ya viongozi wa Mkoa huo na Wilaya ya Meatu wakiondoka eneo la mradi wa maji wa Itinje mara baada ya kukagua mradi huo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji wilayani Meatu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Ndg.Fabian Manoza akitoa maelezo juu ya mradi wa Lubiga wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ya kukagua miradi ya maji wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akihoji jambo juu ya ujenzi wa tanki katika mradi wa Maji wa Itinje wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji wilayani Meatu.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe.Dkt.Joseph Chilongani akifafanua jambo wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ya kukagua miradi ya maji wilayani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...