Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewataka wadau na mashirika mbalimbali wanaofanya kazi na Mkoa huo katika sekta ya Afya kuelekeza fedha zao zaidi katika masuala yanayojibu mahitaji ya wananchi wa Mkoa huo kwenye Afya badala ya kujikita zaidi katika kugharamia mafunzo na semina kwa watumishi.
Mtaka ameyasema hayo katika kikao kilichofanyika Februari 26, Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya mchango wa fedha za wahisani na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya mkoani Simiyu na matokeo yake katika mahitaji halisi ya Kiafya kwa wananchi.
Mtaka amesema mkoa huo una wadau wengi wanaounga mkono juhudi za Serikali katika sekta Afya na wanatoa fedha nyingi ambazo zikiwekwa pamoja na fedha zinazotengwa na Serikali kupitia bajeti za Halmashauri zinaweza kujibu mahitaji ya mkoa huo ambayo ni pamoja na upungufu wa zahanati na vituo vya Afya
“ Msingi mkubwa wa kikao hiki ni kutaka tufanye tathmini ya fedha zinazotolewa na wadau ndani ya mkoa wetu, kwa mwaka huu kwenye Halmashauri zetu tumetenga Bilioni 33.4 na tuna shilingi bilioni 11 kutoka kwa wadau kwa ajili ya sekta ya afya, hivi ‘impact’(matokeo) ya hizi bilioni 11 iko wapi? Natamani hapa kila mwenye fedha yake atuambie mwaka huu atafanya nini” alisema Mtaka.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi, watendaji katika Sekta ya Afya pamoja na wadau mbalimbali wa Afya mkoani humo katika kikao maalum kilichofanyika kwa lengo la kutathmini mchango wa wadau wa Afya(mashirika mbalimbali yanayofanya kazi na mkoa huo) ambacho kilichofanyika Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akifafanua jambo katika kikao kati ya Viongozi wa Mkoa huo , watendaji wa Sekta ya Afya ngazi ya mkoa na Wilaya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA), Bi. Christine Mwanukuzi Kwayu akichangia jambo katika kikao kati ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya Mkoani humo wakifuatilia mada mbalimbali katika kikao cha tathmini ya mchango wa wadau mbalimbali wa Afya Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...