Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma wawatumikie wananchi kwa uweledi na ustadi bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Februari 26, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya za Masasi na Nanyumbu kwa nyakati tofauti.
Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi aliwasisitiza watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao ipasavyo.Alisema Rais Dkt. John Magufuli amesisitiza watumishi wa umma wawatumikie wananchi bila ya ubaguzi wowote pamoja na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
“Watumishi wa umma lazima mtambue kwamba msimamo wa Serikali ni kuwahudumia wananchi bila ya ubaguzi wa kidini, kiitikadi na kipato.”Waziri Mkuu alisema ni vyema watumishi hao kuanza kujitathmini kwa sababu Serikali haitowavumilia watumishi watakaoshindwa kuwajibika kwa wananchi.
Pia aliwataka watendaji hao kuacha urasimu na wahakikishe kila fedha iliyotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inatumika kama zilivyoelekezwa.Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji hao wawe na mpango wa kuwatembelea wananchi kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 27, 2018.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...