Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi.
Halmashauri
ya Wilaya ya Kishapu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imetoa
sh. milioni 208.5 kwa ajili ya kuwezesha kaya maskini katika kipindi
cha Januari hadi Februari.
Mratibu
wa TASAF wilaya hiyo, Sospeter Nyamuhanga amebainisha hayo jana ambapo
amesema fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya kaya 5959 katika vijiji 78
vilivyopo wilaya humo.Alisema kuwa zoezi hilo limeendelea kupata
mafanikio kutokana na walengwa wengi kufanyia kazi elimu wanayopewa
kuhusu matumizi sahihi ya fedha hizo wanazowezeshwa.
Nyamuhanga
aliongeza kuwa kutokana na ufuatiliaji unaofanyika nyakati tofauti
baadhi ya kaya zimeonesha mabadiliko kimaisha ambapo zimetumia fedha
hizo kuboresha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbali za kujipatia
kipato.
Alifafanua
kuwa katika kaya hizo imebainika kuwa wanufaikaji wameweza kununua
mifugo ikiwemo mbuzi, kondoo na kuku huku wengine wakifanya biashara
ndogondogo.Aidha, alisema baadhi ya walengwa tayari wamebadilisha aina
za makazi yao kutoka nyumba za tembe na nyasi za awali na kuanza kujenga
nyumba za kisasa za bati hali inayoleta matumaini katika miradi kama
hii.
“Lengo
la mpango wa TASAF siku zote ni kuziwezesha kaya maskini kujikwamua
kiuchumi na ndiyo maana mara kwa mara katika mazoezi haya tunatoa elimu
ili kuwaelekeza namna bora kutumia fedha wanazowezeshwa,” alisema.
Zoezi
la uwezeshaji Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) likiendelea katika
kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo ambapo mmoja wa walengwa akiwawezeshwa
ruzuku.
Mratibu
wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Sospeter Nyamuhanga (wa pili
kulia waliosimama) akipata maelezo kuhusu zoezi hilo alipofika kufanya
ufuatiliaji kijiji cha Wela kata ya Uchunga.
Sehemu ya walengwa wa TASAF wakiwa katika zoezi la uwezeshaji kwenye kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...